Header Ads Widget

BENKI YA CRDB YAWAITA WACHIMBAJI KUCHUKUA MIKOPO KUENDESHA SHUGHULI ZAO

 


 Na Shomari Binda-Musoma

BENKI ya CRDB imesema inazo fedha za kutosha na kuwaita wachimbaji kwenda kukopa na kuendesha shughuli zao za uchimbaji.

Hayo yamesemwa na Meneja Mahusiano Mwandamizi Madini wa benki hiyo kutoka makao makuu Constancia Makule wakati akitoa mada kwenye kongamano la maonyesho ya madini mkoa wa Mara kwenye ukumbi wa Mwembeni Complex leo juni 5,2025.


Amesema kwa sasa sekta hiyo ya madini inatambulika zaidi ikiwemo shughuli zake na zipo fedha wanazozitoa źa mikopo katika kuboresha kazi zao.

Katika kongamano hilo lililowashirikisha wachimbaji,wauzaji,wachenjuaji na wadau wengine meneja huyo amewaita kuchangamkia fursa hiyo.

Amesema fedha zipo na kikubwa ni kufuata taratibu zikiwemo taarifa sahihi ambazo zitapelekea kupata mikopo hiyo kwa haraka.

" Ndugu zangu benki ya CRDB inazo fedha za kutosha kwaajili ya kutoa mikopo kwa wachimbaji na wadau wote wa sekta ya madini.

" Tumetoka makao makuu na wenzetu wa hapa mkoa wa Mara kuja kuwafikishia ujumbe huo kupitia kongamano hili la maonyesho ya madini mkoa wa Mara", amesema.

Meneja wa CRDB tawi la Musoma Jerome Mwenda amesema wapo tayari kuwapokea wachimbaji na wadau wote wa sekta ya madini ili kuanza michakato ya utoaji mikopo hiyo.

Amesema kama alivyoeleza Meneja Mahusiano Mwandamizi Madini fedha zipo za kutosha hivyo wachimbaji na wadau wa madini wafike na kuzichukua.

Kwenye kongamano hilo wadau wa sekta ya madini pamoja na taasisi za kifedha ikiwemo benki ya CRDB wamekuja na mapendekezo zikiwemo taarifa sahihi zitakazowezesha kupata mikopo.


Licha ya taarifa hizo ni wachimbaji kuhakikisha migao yao ya fedha za mgao wa uuzwaji wa madini ikiwemo dhahabu yanapitia benki.

Kongamano la maonyesho ya madini mkoa wa Mara yameingia siku ya pili hii leo ambapo kesho maonyesho hayo yatafungwa rasmi na Waziri zwa Madini Antony Mavunde kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI