Afisa Udhibiti Ubora (TBS), Bw. Abdul Ngozoma akitoa elimu kuhusu masuala ya viwango kwa wananchi na wajasiriamali waliohudhuria na kutembelea Banda la TBS katika maonesho ya 12 ya Biashara na Utalii yaliyofanyika katika viwanja vya Mwahako City Garden Mkoani Tanga.
Bw. Ngozoma aliwaasa wajasiriamali kujitokeza kwa wingi kuthibitisha ubora wa bidhaa zao kupitia TBS kwani ni sehemu na juhudi ya Shirika kuwasaidia wajasiriamali wadogo bila malipo, hatua inayolenga kuongeza ushindani wa bidhaa zao sokoni na kulinda afya ya walaji.
Na Mwandishi Wetu.
Shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) limeshiriki katika Maonesho ya 12 ya BIASHARA na UTALII yanayofanyika Viwanja vya Mwahako Tanga . Maonesho hayo yalianza Tangu Mei, 28 na yatahitimishwa June , 06 , 2025 yakiwa na Kauli mbiu " MUONEKANO WA WADAU SEKTA YA UMMA NA BINAFSI KWENYE UWEKEZAJI , UKUAJI NA UENDELEVU WA BIASHARA".
TBS wametumia Maonesho hayo kutoa elimu kwa Umma kuhusu umuhimu wa Viwango , lakini pia imewatembelea wazalishaji wadogo na kuwaelezea kuhusu umuhimu wa kuwa na alama ya ubora katika bidhaa wanazozizalisha.
0 Comments