Header Ads Widget

ZELENSKY AKARIBISHA VIONGOZI WA ULAYA UKRAINE KATIKA JUHUDI ZA KUKOMESHA VITA

 


Viongozi wa Ulaya wako mjini Kyiv nchini Ukraine katika juhudi za usitishaji mapigano.

Mkutano huu unawadia baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer kutangaza vikwazo vipya kwa kile Putin alichokiita “shadow fleet” hapo jana.

Neno hili linarejelea kundi la meli za mafuta za Urusi zenye kuhusishwa na vikwazo vya usafirishaji wa mafuta na gesi.

Akijibu, Zelensky alisema siku ya Ijumaa kwamba anashukuru Uingereza kwa "vikwazo vipya" vyenye uzito.

"Kila hatua ambayo inazuia uwezo wa Kremlin kufadhili vita vyake huleta amani karibu. Uingereza kwa mara nyingine tena inaonyesha mbinu ya uongozi," alisema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI