Na Happiness Shayo, Makambako
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi Dkt.Pindi Chana (Mb) ameshiriki katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Shule ya Msingi Idofi kwenye Kijiji cha Idofi, Halmashauri ya Mji wa Makambako, Mkoani Njombe leo Mei 3,2025.
Akizungumza katika mapokezi hayo, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka amesema Mwenge huo utakimbizwa jumla ya kilomita 869.7 kwa muda wa siku sita katika Wilaya nne za Mkoa wa Njombe ambapo utazindua, kukagua, kufungua, kugawa na kutembelea jumla ya miradi 62 yenye thamani ya shilingi bilioni 17.6 Mkoani humo.
Mwenge huo uliongozwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 Bw. Ismail Ali Ussi kutoka Unguja Kaskazini.
0 Comments