Na Matukio Daima Media
Kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, waandishi wa habari nchini wametakiwa kuzingatia misingi ya ukweli, uwazi na kutokuegemea upande wowote wa kisiasa katika kuchapisha taarifa za habari, ili kulinda amani na kuimarisha demokrasia.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Program wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Paul Malimbo, wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na mtandao wa watetezi wa haki za binadamu tanzania (THRDC).
katika maelezo yake, Malimbo amesema kuwa baadhi ya waandishi wamekuwa wakimtegemea chanzo kimoja cha taarifa bila uthibitisho wa kina, huku wengine wakimtumia akili mmemba kama chanzo cha habari jambo linalopelekea kupokea taarifa zisizo za kweli.
‘’Kumekuwa na misukosuko mingi kwa wandishi wa habari haswa katika kipindi cha uchaguzi na sisi tumekuwa tukipokea kesi nyingi za waashindi wa habari wakikamatwa katika kipindi hiki sasa katika kuelekea uchaguzi wa mwaka huu waashindi tujitahidi kuandika habari ambazo zinaukweli saivi tumeshuhudia waandishi wengi wakitumia Akili Mmemba katika kuandaa habari, habari ambazo muda mwingine sio za kweli lakini pia katika kufuata maadili ya uandishi ni vizuri kutotumia vyombo vyetu vya habari katika masuala ya kisiasa.
Aidha Mkurugenzi wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Keneth Simbaya, amesema waandishi wa habari wanapaswa kufahamu sheria na kanuni za taaluma yao, pamoja na kuwa na mshikamano katika kutetea haki zao na maadili ya kazi wanazofanya.
“Waandishi wengi tumekuwa tunaandika sana habari za watu lakini hatuandiki habari za kwetu na wala hatujitetei kabisa na hapo ndipo tunapopigiwa sisi waandishi, na hii ni kwasababu hatufuatilii kabisa sheria na kanuni zinazotuongoza katika misingi ya habari hizi sheria zilizopo ni za muda mrefu na zinahitaji mabadiliko lakini sijaona press klabu hata moja ikimwita hata Mbunge kwaajili ya mabadiliko ya sheria zetu ambazo sisi kama waandishi tunaona ni kandamizi ”
Kwa upande wake Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Onesmo Ole Nguruma amewataka wanahabari kutumia nguvu yao ya ushawishi katika jamii kwa kuwa na ajenda moja kwa kuisimamia na kuifanya kuwa ajenda ya kitaifa yenye maslahi kwa umma.
Hata hivyo Ole Ngurumwa amekemea vikali vitendo vya utekaji watu na kuumizwa wakati huu wa Uchaguzi na kutaka serikali kukemea
“Waaandishi wa habari wana nguvu sana lakini kwa kipindi hiki hizo nguvu hawazitumii kipindi cha nyuma waandishi walikuwa na nguvu sana na walikuwa wakizitumia hizo nguvu kwa kuamka na ajenga ambazo wanazishilikilia na zinafanyiwa kazi lakini kwa sasa waandishi wa habari ndo wanapewa ajenda na za kuandika .
0 Comments