Header Ads Widget

WAFUGAJI KILWA SOKO SASA NI UHAKIKA

 

NA HADIJA OMARY 

Zaidi ya shilingi milioni 106 zinatarajiwa kutumika Katika ujenzi wa Mnada wa mifugo Katika kijiji cha njinjo Wilayani Kilwa  na kuwawezesha wafugaji kupata soko la uhakika 

Mradi huo umewekewa jiwe la Msingi Leo mai 31, 2025 na kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2025 Ismail ally usi ambapo ame9nyesha kuridhishwa na Hatua ya halmashauri kuanzisha Mradi huo ambao utakuwa na tija kwa wananchi

Ujenzi wa Mradi wa Mnada wa mifugo unataraji kutekelezwa kwa awamu mbili ambapo kwa awamu hiyo ya Kwanza unahusisha ujenzi wa ukuta, mageti na pakilio huku awamu ya pili ikihusisha ujenzi wa vyoo, kibanda cha mlinzi na mtoa ushuru pamoja na uwekaji wa taa
Mradi huo utakuwa na manufaa mbalimbali kwa wananchi ikiwa pamoja na kuongezeka kwa mapato ya kijiji, halmashauri na Serikali kuu kupitia Ada na tozo, kuwepo kwa soko la mifugo la uhakika kutokana na ushindani wa manunuzi, kusaidia Katika udhibiti ya wagonyama na kuzuia upotevu wa mifugo

Mbunge wa Jimbo la kilwa kaskazini France ndulane Amesema Hatua ya halmashauri kuanzisha ujenzi huo wa jengo la Mnada wa mifugo ni kutokana na uwepo wa wafugaji ambao walihamia kutoka Maeneo mbali mbali hapa Nchi 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI