Na Shomari Binda-Tarime
WAANDISHI wa Haɓari mkoani Mara wameahidi kumpa ushirikiano wa kutosha mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi kwa kutangaza mazuri ya mkoa huo.
Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mara Jacob Mugini amemuomba mkuu wa Wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele kumfikishia salamu mkuu huyo wa mkoa kuhusu ushirikiano huo.
Kauli hiyo ameitoa jana mei 23,2025 kwenye ukumbi wa CMG Hotel mjini Tarime wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kwa mkoa wa Mara.
Amesema mkoa wa Mara unazo fursa nyingi ambazo zinapaswa kutangazwa na kupitia kalamu zao na kamera wataendelea kuzitangaza.
Mugini amesema Waandishi wa mkoa wa Mara kwa sasa wapo mstari wa mbele kuyatangaza mazuri yote ili kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza mkoa wa Mara na kuacha story zenyte ukakasi.
" Mheshimiwa mkuu wa Wilaÿa tunaomba utufikishie salamu zetu kwa mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi kwamba tupo tayari kumpa ushirikiano wote katika kutangaza fursa za mkoa wetu.
" Tunayo maeneo mazuri ya uwekezaji ikichangizwa na hali nzuri ya usalama ya mkoa wa Mara hivyo tupo tayari kufanya kazi ya kuelezea dunia",amesema.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo mkuu wa Wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele amesema atamfikishia salamu hizo mkuu wa mkoa kuhusu ushirikiano waliomuahidi.
Licha ya kuahidi kufikisha salamu hizo amewataka Waandishi wa Habari mkoani Mara kufanya kazi zao Ä·wa maadili na kuepusha migogoro ya kihabari.
Aidha mkuu huyo wa Wilaya amemtaka kila Mwandishi anayemiliki mitandao zikiwemo blog na Online Tv kuhakikisha wanazisajili kwa kuzingatia Sheria ili kufanya kazi kwa uhuru.
Katika maadhimisho hayo klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mara(MRPC) imewapa motisha wanahari waliofanya vizuri kwa kutoa elimu na taarifa kwa jamii.
0 Comments