Na WILLIUM PAUL, MOSHI.
MRADI wa Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Amali Manushi unaendelea katika Kijiji cha Manushi Sinde.
Mpaka sasa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 73 ambapo ujenzi unaoendelea ni wa Majengo 8 ya Madarasa, Jengo la Utawala, Maktaba, Maabara tatu za Sayansi, jengo la Tehama na vyoo vya Wasichana na Wavulana.
Serikali inawashukuru Wananchi wa Vijiji vya Manushi kwa kukubali kutoa eneo la ekari 20 kwa ajili ya ujenzi huo.
Kiasi cha shilingi 584 milioni kimetolewa na Serikali kwa kazi hiyo ambapo wananchi wameishukuru Serikali kwa kufadhili mradi huo.
Pia wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi na Diwani wa Kata ya Kibosho Magharibi, Prosper Massawe kwa kuupigania mradi huu.
Mwisho.
0 Comments