Na Shomari Binda-Musoma
KATIBU wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM mkoa wa Mara Baraka Mwachula amesema uhai wa jumuiya hiyo ni ulipaji wa ada na kufanya vikao.
Hayo ameyasema leo mei 19,2025 alipokuwa akizungumza na viongozi wa jumuiya hiyo Wilaya ya kichama ya Musoma vijijini kwenye ukumbi wa Wilaya uliopo Murangi.
Amesema pasipo kulipa ada na kufanyika kwa vikao uhai hauwezi kuwepo na kuwezesha kufanya shughuli za jumuiya na chama.
Mwachula amesema panapofanyika vikao kunawezesha kujadiliana masuala mbalimbali na kusaidia kuijenga jumuiya.
Amesema ulipaji ada ni msingi na kumfanya mwanachama kuthamini uanachama wake na kusisitiza umuhimu wa kulipia ada ya jumuiya na chama.
Kuelekea uchaguzi mkuu Katibu huyo amewataka viongozi wa jumuiya hiyo Musoma Vijijini kujiandaa na kuwashawishi wale wanaowaona wanafaa kuomba nafasi ya uongozi
Amesema kwa upande wa mgombea wa nafasi ya Rais tayari yupo mgombea Dkt.Samia Suluhu Hassan na kuwataka kwenda kumsemea kutokana na maendeleo makubwa aliyoyafanya.
Licha ya kuwashawishi wagombea kwenye nafasi za udiwani na ubunge wawaache waendelee na michakato wenyewe kuliko kuambatana nao na kujiepusha kuwachagua viongozi kwa kigezo cha kutoa Rushwa.
Katika suala la maadili kwa watoto amesema jumuiya ya nwazazi ndio walezi na wasimamizi wa watoto hivyo ni vyema kwenda kusimamia suala la maadili.
Katibu huyo wa mkoa amempongeza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Musoma Vijijini Nyakia Nyakia kwa kusimamia vyema jumuiya hiyo.
Amesema mahudhurio ya Kata 20 kati ya 21 kwenye kikao ni ishara ya kuonyesha namna bora ya usimamizi wa jumuiya na kazi zinafanyika.
Kwa upande wa viongozi wa wilaya hiyo waliohudhuria kikao hicho kupitia Mwenyekiti Nyakia Nyakia wamesema wamepokea maelekezo yaliyotolewa na wanakwenda kuyafanyia kazi.
Aidha Katibu huyo wa mkoa amefanya pia ziara Wilaya ya Musoma mjini hii leo na kuzungumza masuala mbalimbali ambapo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma mjini Magiri Benedict alipata nafasi ya kuzungumza na kueleza wajumbe wa jumuiya ya wazazi kuhakikisha wanachangia na kupata nyumba ya mtumishi
0 Comments