Mkutano uliokusudiwa kutuliza mvutano kati ya Marekani na Afrika Kusini badala yake mvutano uliongezeka huku Rais Donald Trump akimweka mwenzake kwenye utetezi kwa madai kwamba wakulima wa kizungu katika taifa lake walikuwa "wakinyanyaswa" na kuuawa
Siku ya Jumatano, wiki moja baada ya Marekani kuwapa hifadhi karibu Waafrikana 60, hatua iliyoikereketa Afrika Kusini, Rais Cyril Ramaphosa alitembelea Ikulu ya White House kurejesha uhusiano wa nchi hizo.
Badala yake, Trump alimshangaza Ramaphosa wakati wa mkutano wa waandishi wa habari wa moja kwa moja na madai yaliyokanushwa sana ya "mauaji ya kimbari" nchini Afrika Kusini.
Alicheza video inayoonesha wakati wa maandamano ya misalaba kadhaa iliyopanga Barabara, akidai kuwa ni maeneo ya kuzikia wakulima wazungu waliouawa.
Trump alisema hajui ilirekodiwa wapi nchini Afrika Kusini. Misalaba, kwa kweli, si makaburi halisi, lakini inaonekana ni wakati wa maandamano ya 2020 baada ya wanandoa wakulima kuuawa katika jimbo la KwaZulu-Natal. Waandalizi walisema wakati huo kuwa ni maonesho yanayowakilisha wakulima waliouawa kwa miaka mingi.
Kabla ya mkutano wa Jumatano wa White House, kiongozi wa Afrika Kusini alisisitiza kuwa kuboresha uhusiano wa kibiashara na Marekani ndio kipaumbele chake. Mauzo ya bidhaa za Afrika Kusini kwenda Marekani yanakabiliwa na ushuru wa asilimia 30.
Ramaphosa alitarajia kumvutia Trump wakati wa mkutano huo, akileta wachezaji wawili mashuhuri wa gofu wa Afrika Kusini na kumpa zawadi ya kitabu kikubwa kinachooyesha viwanja vya gofu vya nchi yake.
Mkutano huo umekuja siku chache baada ya Waafrika Kusini 59 wazungu kuwasili Marekani, ambako walipewa hadhi ya ukimbizi. Ramaphosa alisema wakati huo walikuwa "waoga".
0 Comments