Header Ads Widget

WAFANYAKAZI WAWILI WA UBALOZI WA ISRAEL WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI MAREKANI

 

Wafanyakazi wawili wa ubalozi wa Israel wameuawa nje ya jumba la makumbusho la Wayahudi katikati mwa jiji la Washington DC, maafisa wanasema.

Waathirika, mwanaume na mwanamke, walipigwa risasi walipokuwa wakitoka kwenye hafla katika Jumba la Makumbusho la Capital Jewish, duru ziliiambia mshirika wa BBC CBS, na kuongeza kuwa tukio hilo linaonekana kupangwa.

Shambulizi la risasi lilitokea saa 21:05 kwa saa za huko karibu na 3rd na F Streets NW, eneo lenye maeneo mengi ya watalii, makumbusho na majengo ya serikali, ikiwa ni pamoja na ofisi ya FBI ya Washington.

Ripoti zinaonesha kuwa wafanyakazi wengi wa ubalozi wa Israel walikuwa kwenye hafla ya makumbusho wakati wa ufyatuaji risasi.

"Wafanyakazi wawili wa Ubalozi wa Israel waliuawa usiku wa kuamkia leo karibu na Jumba la Makumbusho la Kiyahudi huko Washington DC," mkuu wa Usalama wa Ndani wa Marekani Kristi Noem alichapisha kwenye X.

"Tafadhali tuombe kwa ajili ya familia za waathirika. Tutamfikisha mbele ya sheria mhalifu huyu mpotovu." Balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa amelitaja tukio hilo kuwa "kitendo potovu cha ugaidi dhidi ya Wayahudi".

"Kudhuru wanadiplomasia na jumuiya ya Wayahudi inavuka mstari mwekundu," Balozi Danny Danon aliandika kwenye X.

"Tuna uhakika kwamba mamlaka za Marekani zitachukua hatua kali dhidi ya wale waliohusika na kitendo hiki cha uhalifu."

Tukio hilo lilizua mwitikio mkubwa wa polisi na kufunga mitaa kadhaa ya jiji.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI