Header Ads Widget

WAGAZA WAHOFIA KUFUNGWA KWA MITAMBO YA MAJI HUKU ISRAEL IKIZIDISHA MASHAMBULIZI

 

Uhaba wa maji unaoendelea Gaza unazidi kuwa mbaya huku mashambulizi ya kijeshi ya Israel yakizidi kusababisha wimbi jipya la watu kuyahama makazi yao na mitambo ya kuondoa chumvi na usafi wa mazingira inakosa mafuta.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kibinadamu imesema washirika wake wanaonya kwamba, kukosekana kwa mafuta mara moja kutasababisha kufungwa kwa maji na huduma za vyoo mwishoni mwa juma.

Siku chache baada ya Israel kuweka vikwazo vya misaada mapema mwezi Machi ambayo sasa inapunguzwa, pia ilikata nyaya za umeme kwenye mitambo mikuu ya kuondoa chumvi, chanzo muhimu cha maji kwa Wagaza.

Ilisema hatua hizi ni kuweka shinikizo kwa Hamas kuwaachilia mateka waliosalia.

Ingawa Israel imesema sasa itaruhusu kuingia kwa mahitaji ya msingi katika Gaza, hadi sasa hii haijajumuisha mafuta.

Hata hivyo, baadhi ya maji ya kunywa yalipakiwa kwenye malori mengi ya Umoja wa Mataifa ambayo yameingia kwenye ukanda huo na vifaa bado havijasambazwa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI