Header Ads Widget

TLS YABAINI UVUNJWAJI WA SHERIA NA KATIBA KWA POLISI MAHAKAMANI.


 Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika -TLS katika kufuatilia suala la Jeshi la Polisi kuwazuia na kukamata raia Mahakamani Aprili 24 na 28 mwaka huu Mahakama ya Kisutu, tumebaini uvunjwaji wa sheria na Katiba) kama ifuatavyo:

(i) Uvunjaji wa haki ya usawa mbele ya sheria; kukamatwa kwa wananchi kwa wingi katika Mahakama ya Kisutu tarehe 24/04/2025 bila kufuata msingi wa kisheria na kwa kuonekana kuzingatia misimamo ya kisiasa ni kinyume na Ibara ya 13 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inayolinda usawa mbele ya sheria na kupinga ubaguzi wa kisiasa, Ibara ya 14 ya Katiba inayolinda haki ya kila mtu kuishi na kulindwa na serikali na jamii,

(ii) Uvunjaji wa haki ya uhuru wa mtu binafsi; wote waliokamatwa katika viunga vya Mahakama walinyimwa haki yao ya uhuru kama inavyolindwa na Ibara ya 15, kukamatwa huko kulitokea bila sababu za kisheria, bila hati ya kukamatwa, wala kufuata taratibu za sheria,

(iii) Uvunjaji wa haki ya uhuru wa mtu kwenda atakako; matendo ya Jeshi la Polisi la Tanzania tarehe 24/04/2025 na 28/04/2025 yalizuia watu kuhudhuria kwa uhuru uendeshaji wa kesi kwenye Mahakama ya wazi, kinyume na Ibara ya 17 ya Katiba,

(iv) Kutotekelezwa kwa taratibu za sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai; vitendo vya vyombo vya ulinzi na usalama vilikiuka kifungu cha 186 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, toleo la 2022 kinachothibitisha uwazi wa vikao vya Mahakama, aidha vifungu vya 11, 12, 14, 21, 23 na 54 vilikiukwa kwa:-

a.) kukamata watu bila kuwafahamisha makosa yao, b.) kukosa kuwasilisha hati halali za kukamatwa, c.) kuwanyima waliokamatwa haki ya kuwasiliana na Wakili au jamaa zao, d.) kutumia nguvu kupita kiasi na kusababisha majeraha makubwa, na e.) kufanya upekuzi na ukamataji bila kufuata sheria katika makazi ya mtuhumiwa terehe 28/04/2025 ambapo familia ya mtuhumiwa iliweza kuzuia uvunjifu huo,

matukio ya terehe 24/04/2025 na 28/04/2025 yalidhihirisha ukiukwaji wa haki ambapo baadhi ya viongozi wa CHADEMA walizuiwa kwa nguvu kuhudhuria kesi hiyo, jambo ambalo ni kinyume na kifungu cha 186 kinacholinda haki ya wananchi kushiriki katika kesi zinazotakiwa kuendeshwa katika mahakama ya wazi" Mwabukusi


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI