Header Ads Widget

MASHIRIKA YA KUTOA MSAADA GAZA YANAMALIZA CHAKULA MIEZI MIWILI TANGU ISRAEL KUFUNGA VIVUKO VYOTE

 

Imekuwa vigumu mlo kupatikana katika Ukanda wa Gaza, lakini chakula cha mchana kwa familia zenye mahitaji kusini kinakaribia kuwasilishwa kwa punda na mkokoteni.

Mlo wa leo ni koshari - uliotengenezwa kwa dengu, wali na mchuzi wa nyanya - ukiwa umefadhiliwa na Shirika la kutoa misaada ya kibnadamu la Wakimbizi la Marekani (Anera).

"Watu wanategemea milo yetu; hawana chanzo cha mapato kununua kile kilichosalia katika masoko ya ndani na vyakula vingi havipatikani," anasema Sami Matar, ambaye anaongoza timu ya Anera.

"Hapo zamani tulikuwa tukipika wali na nyama - na protini. Sasa, kwa sababu kumefungwa, hakuna nyama, hakuna mboga mboga zinazotoka shambani."

Miezi miwili iliyopita, Israel ilifunga vivuko vyote kuelekea Gaza - kuzuia bidhaa zote, ikiwa ni pamoja na chakula, mafuta na madawa kuingia - na baadaye ilianza tena mashambulizi yake ya kijeshi, na kumaliza usitishaji wa mapigano wa miezi miwili na Hamas.

Ilisema hatua hizi zilikusudiwa kuweka shinikizo kwa Hamas kuwaachilia mateka ambao bado inawashikilia.

Hivi karibuni, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani na shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi wa Kipalestina, walisema wametumia akiba yao yote ya chakula cha msaada.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI