Header Ads Widget

TET NA VYUO VYA UDOM, PANTANNDI WASHIRIKI SEMINA YA MRADI WA "LEARNING IS VISUAL"



 Semina ya kuhitimisha mradi wa Elimu uitwao "learning is visual" ambao umedumu kwa miaka minne tangu mwaka 2022 hadi sasa, ambapo semina hiyo imewakutasha wadau kutoka chuo cha Patanndi,  Chuo cha Dodoma, Taasisi ya Elimu Tanzania pamoja na washirika wa mradi kutoka Norway

Akizungumza baada ya kushiriki siku ya kwanza ya semina hiyo ambayo inafanyika kwa siku mbili katika hotel ya Protea tarehe 27 na 28 mwaka 2025, Mwl. Rusiani Eleoseni Segesera ambaye ni Mkuu wa chuo cha Patandi amesema mradi huo umekuwa wenye manufaa makubwa kwa watanzania na wadau wa Elimu kwa ujumla, akijaribu kutoa tathimini ya kile kilichofanyika kuhusiana na mradi huo ambao wadau wakubwa ni chuo kutoka Norway 

Aidha, Segesera amesema kuwa mradi umewanufaisha wanafunzi wenye mahitaji maalum kama wenye uoni hafifu, wasioona kabisa na wengine na kuongeza kuwa wanafunzi wenye changamoto ya uoni wananufaika kwa kununuliwa vifaa ambavyo vitakavyo wasaidia kwenye uoni pamoja na walimu wao kupata fursa ya kusomeshwa na Serikali



Kwa upande wake Jackline Masawe ambaye ni mtaalamu wa Elimu maalum upande wa wasioona ameshukuru kushiriki semina hiyo na kukiri kwamba yeye ni mnufaika makubwa wa mradi huo tangu mwaka 2018 mradi huo ulipoanza

"2018 nikipata Elimu ya namna ya kupima na kuwafanyia mazoezi ya utengamao watoto wenye mahitaji maalum wenye uoni hafifu pamoja na macho kuona upande mmoja, macho kuacha kuzunguka kwa kawaida, kwaiyo nimefaidika sana na hii programu na ndio maana nipo hapa".

Hata hivyo Dkt. Abdalla Jacobo  Seni ambaye ni Kaimu Rasi ndaki ya Elimu katika chuo kikuu cha Dodoma amesema katika mradi wa "learning is visual" wameweza kutengeneza "degree progaram ya masters" katika maswala ya mahitaji maalum na kutanabaisha kwamba vijana wengi wameweza kupewa ufadhili ambapo zaidi ya wanafunzi 43 wamepata ufadhili wa shahada ya uzamivu





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI