Header Ads Widget

TDB -TUMIENI MAZIWA YALIYOSINDIKWA


Na Matukio Daima Media

BODI ya Maziwa Tanzania(TDB) imeitaka jamii kuacha kununua maziwa ya ngo'mbe holela yanayouzwa kwenye chupa za plastiki   na badala yake watumie maziwa salama na yaliosindikwa kwa afya bora. 

Rai hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam leo Mei 20, 2025 na Mwakilishi wa Msajili wa  wa bodi ya Maziwa Deorinidei Mna'ona'o wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuelekea Kilele cha wiki ya kitaifa ya Maziwa inayotarajia  kufanyika Mei, 27 hadi Juni Mosi mwaka huu Mkoani Morogoro.


Amesema maziwa ya Ngo'mbe yanayouzwa mtaani kwenye chupa usalama wake ni mdogo mno  kutokana kuwekwa katika mazingira yasiyo salama kwa afya ya  mlaji.

"Tumekuwa tukiamasisha unywaji wa maziwa salama na yaliosindikwa..maziwa  yanayouzwa mtaani ni hatari sana  kwani yamekuwa yakiwekwa katika mazingira  yasiyo salama kwa afya ya mlaji."amesema 

Amesisitiza kuwa maziwa ni chakula chenye virutubisho na kueleza kuwa yanapowekwa katika mazingira yasiyo salama ufuatwa na vijidudu jambo  ambalo ni hatari kwa mlaji na mfanyabiashara pia.

 Amesema  kuwa bodi hiyo imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali ikiwemo kutoa elimu na kuamasisha wafugaji kupata mbegu bora.


Aidha aliwaomba waandishi wa habari kupitia mafunzo hayo kupeleka elimu sahihi kwa jamii juu ya matumizi ya Maziwa salama.

Kwa upande wake Ofisa Jinsia Lishe, Ruth Mkope amesema maziwa ya ngo'mbe yanavirutubisho vya aina nyingi  hivyo huweza kuwa mlo kamili kwa watu wote.

"Unywaji wa maziwa inapaswa kupewa msukumo kwa watoto wa shule wenyewe bila kutegemea wafadhili"amesema 

Amesema kwa upande wa mtoto maziwa ni chanzo cha virutubisho vingi vinavyohitajika kwa ajili ya ukuaji na maendeleo yake.

"Maziwa usaidia kuimarisha kinga ya mwili ya mtoto lakini maziwa ya wanyama hayatumiki kwa watoto chini ya mwaka mmoja "alisisitiza Mkope 

Aidha amesema Shirika la Afya linashauri unywaji wa lita 200 kwa mtu mmoja kwa mwaka sawa na mililita 500 kwa mtu mmoja kwa siku.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI