Header Ads Widget

SHEIKHE RAJABU 'AWANANGA' WATUMIAJI WA HOVYO WAMITANDAO YA KIJAMII

 

Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima App Dodoma

SHEIKHE wa Mkoa wa Dodoma,Alhaj Dkt Mustapha Rajabu Shaaban amewataka Waandishi wa Habari kufuata miiko ya uandishi wa habari huku akiwataka watumiaji wa mitandao kuchuja habari kabla ya kulike,Comment na kushare.

Kauli hiyo ameitoa leo Mei 30,2025 Jijini hapa katika Ibada ya swala ya Ijumaa iliyofanyika katika msikiti wa Gaddafi Jijini hapa ambapo Sheikhe Rajabu amesema vyombo vya habari vina athari kubwa iwapo havitatumiwa vizuri na Waandishi wa Habari ikiwemo kuondoa amani ya Nchi.

"Waandishi wa Habari wakitumia hivyo vyombo vyao vya habari katika kujenga umma basi utafanikiwa iwapo watatumia artical zao katika yale ambao ni sahihi.Na endapo watatumia vibaya ni rahisi kuupotosha umma au kuharibu heshima ya mtu, habari unavyoipeleka ni  lazima uihakiki,"amesema Sheikhe Rajabu

Pia amewataka watumiaji wa mitandao kuchuja aina ya Habari kabla ya kuishare,kulike na kucoment.

"Je taarifa hii inaenda  kujenga  ama kubomoa na sisi tunaofikishiwa lazima tuchuje  sio tuna like kushare na kucoment 

Amesema Mwandishi na mpokeaji wote  tunatakiwa kufuatia misingi ili kuhakikisha kile wanachotuma kinakuwa hakina madhara katika jamii.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI