Header Ads Widget

RC SERUKAMBA ATANGAZA KUGOMBEA UBUNGE

 

Na Matukio Daima App.

IRINGA.Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba, ametangaza rasmi dhamira yake ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao, akisema sasa ni muda wa kuwatumikia Wananchi kwa ukaribu zaidi kupitia nafasi ya uwakilishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingawa bado hajaweka wazi atagombea Jimbo lipi.

Serukamba amesema hayo wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, kilicholenga kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.

“Mimi leo nadiriki kusema nadhani hii ni Halmashauri yangu ya Mkoa ya mwisho na Mimi nimekata shauri namuonea wivu Kaka yangu Lukuvi kukaa Bungeni muda mrefu na Mimi nataka niende hukohuko, na nina uhakika nitashinda huko ninakoenda, nawashukuru sana na wale wote mnaokwenda kugombea nawatakia kila la kheri “

 Akizungumza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Daud Yassin alisema kuwa ni faraja kwa Mkuu huyo kuwa ni kikao chache cha halmashauri cha mwisho japo wanasikitika kumpoteza.

"Serukamba tumeshirikiana nae vizuri sana ni mshauri mzuri, mkweli, kama mnakumbuka aliwahi kusema kitu ambacho hakitaki ni majungu,mtu akienda kwake aende na habari za ukweli tu na kipindi chote ambacho tumefanya nae kazi ushauri wake kwenye chama umekuwa ukitusaidia sana"

Yassin alisema kuwa kwa namna walivyokuwa wanashirikiana watamkumbuka kwa mazuri aliyowashauri, hivyo hawana budi kumuombea akashinde huko ambako anaenda kugombea.

"Kwaniaba ya Halmashauri kuu tunamtakia kila la kheri na kuwa huko anakoenda akafanikiwe na tunatarajia hata kama unaondoka ushirikiano wetu utaendelea"

Aidha aliwataka viongozi wote kutenda haki na kuacha kudhurumu haki za watu ukiacha udiwani ambao wanamalizia katika mkoa huo katika ngazi ya Ubunge wao kama viongozi wanajukumu la kupendekeza wagombea tu.

"Tunaweza kupendekeza majina matatu kufika Dodoma yakaondolewa yote akapendekezwa mtu ambaye hatukumtarajia,Mungu atatusaidia tutavuka salama katika uchaguzi huu"

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI