Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew amewasili kata ya Gilya wilayani Bariadi Mkoa I Simiyu kwa ajili ya kufanya Mkutano Maalumu wa kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020/2025.
Akiwa kwenye kata hiyo, Mhandisi Kundo atagawa vifaa vya michezo kwenye Matawi ya Gilya, Nyawa, Mwauchumu, Ikinabushu na Isuyu ambapo kila tawil litapewa mipira minne na jezi moja ya jezi wakati huo kata ya Gilya ikipatiwa Mipira mitatu na jezi pea moja ili kuunga Mkono jitihada za Rais Dk.Samia kwenye sekta ya michezo.
Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, atagawa pampu nne za Maji ili kuwasogezea wananchi huduma ya Maji huku akiwashukuru wananchi kwa kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Mwisho.
0 Comments