Header Ads Widget

RC NJOMBE:MSIBWETEKE UKIMWI BADO UPO NA UNA UA

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wakati watu sita kati ya 1112 waliojitokeza kupima afya katika mikesha ya mwenge wa uhuru mkoani Njombe wakibainika kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi,Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amewataka wananchi kuacha mizaha kwenye suala la afya kutokana na takwimu hizo.

Wakati wa Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru wa 2025 kati ya Mkoa wa Njombe na Ruvuma katika shule ya Msingi Igawisenga Wilayani Madaba Mkuu wa Mkoa wa Njombe amesema pamoja na Takwimu hizo lakini ipo haja ya wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ukimwi kwani upo na Una uwa.

Awali mkuu wa Wilaya ya Njombe Juma Sweda amesema katika Mkesha wa Mwenge huo kwenye viwanja vya kituo cha mabasi cha Zamani Halmashauri ya Mji wa Njombe mtu mmoja pekee kati ya 177 waliojitokeza kupima afya ndiye aliyegundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Naye Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka huu Ismail Ali Ussi ametumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa mkoa wa Njombe kwa kufanikisha mwenge kuvuka salama katika mkoa huo bila dosari ya mradi wowote huku wakitakiwa kwenda kuwasimamia wananchi na viongozi wa ngazi za chini.



Baada ya Katibu tawala mkoa wa Njombe Judica Omary Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa kumkabidhi mwenge wa Uhuru Katibu Tawala mkoa wa Ruvuma Merry Makondo kwa niaba ya mkuu wa Mkoa huo amesema Jumla ya miradi 76 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 95  itapitiwa katika Halmashauri zote Nane.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI