Header Ads Widget

RC MTAMBI AISHUKURU SERIKALI,WAZIRI MAVUNDE KUWEZESHA VIJANA SEKTA YA MADINI


Na Shomari Binda-Tarime

MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi ameishukuru serikali kupitia Wizara ya Madini na mgodi wa Barrick North Mara kuwezesha vijana uchimbaji wa madini.

Vijana hao kwenye vikundi 48 wamewezedhwa na serikali na mgodi huo kupewa leseni zaidi ya 100 hii leo mei 3,2025 katika uzinduzi mkubwa wa ugawaji awamu ya kwanza uliofanyika shule ya sekondari Ingwe iliyopo Nyamongo.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Mtambi amempongeza Waziri Mavunde kwa namna anavyowasaidia wananchi wa Mara hususan katika eneo la sekta ya Madini ambapo amesema juhudi za Waziri huyo zinaonekana kwa vitendo na kuomba vijana hao wajengewe uwezo ili waweze kuchimba kwa tija.

Sambamba na hayo Kanali Mtambi amemuomba Waziri Mavunde kutoishia kwenye utoaji wa leseni pekee bali pia kuliangalia suala la msaada wa kiufundi pamoja na mitaji ili kuwawezesha wachimbaji hao kufanya kazi kwa tija.

" Nikushukuru sana mheshimiwa Waziri kwa jambo hili kubwa ambalo limefanyika hii leo kwa ushirikiano wa serikali na mgodi kueezesha vijana

" Baada ya kuwezesha leseni ni mujimu sasa waweze kupata mafunzo ambayo yatawawezesha kuchimba kwa tija na kujiinua kiuchumi",amesema.

Waziri wa Madini Antony Mavunde akizungumza kwenye uzinduzi huo amesema Wizara imekamilidha maandalizi ya program ya MBTambayo itatekelezwa katika kipindi cha miaka 5 kuanzia 2025/2030 na kudai program hiyo ni ya kimageuzi katika sekta ya madini.

Amesema mradi huo wa kihistoria ni wa kwanza kufanyika nchini baina ya serikali,mgodi na wananchi wanaozunguka mgodi na umevutia ushiriki mkubwa wa wadsu kama benki ya dunia ( WB)na Baraza la Dhahabu Duniani ( WGC) ambao wameonyesha dhamira ya kusaidia utekelezaji wake.

Meneja Mkuu wa mgodi wa Barrick North Mara Mhandisi Apolinary Lyambiko amesema utoaji wa leseni hizo una lengo la kuimalisha uhusiano mwema na jamii inayozunguka mgodi.

Naye Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA), John Bina amempongeza Waziri Mavunde kwa kuzindua mradi huo na kuwataka vijana, wanawake na wenye mahitaji maalumu kufanya kazi kwa kushirikiana na kuepuka migogoro isiyo ya lazima.

Awali akitoa salamu zake mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara ameoshukuru serikali kupitia Wizara ya Madini kwa tukio hilo ambalo linakwenda kuwasaidia vijana na kuepusha migogoro.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI