Header Ads Widget

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI WA MAJI CHIUMBATI

Na Hadija Omary 

Lindi ina jumla ya wakazi 12,619 kutoka Katika vijiji 11 vya  halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi wanatarakiwa kunufaika na huduma ya maji Safi na salama baada ya mbio za mwenge wa Uhuru kuzindua Mradi mkubwa wa maji Katika kijiji Napanga

Kwa mujibu wa Meneja wa Ruwasa Wilaya ya  Nachingwea mhandisi Ramadhani Musiba Amesema Mradi huo umetekelezwa na mkandarasi Broadadways Engineering co ltd kwa gharama ya zaidi ya Bilioni 1 ambapo mpaka sasa Utekelezaji wake umeshakamilika.


Baadhi ya wananchi wamemshukuru Rais Samia kwa kutoa Fedha za kutekeleza Mradi huo ambao kwa kiasi kikubwa unaenda kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo

Akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua Mradi huo kongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2025 Ismail ally usi amewataka wananchi kuitunza miundombinu hiyo ya maji ili iweze kutumia kwa muda mrefu.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI