Na Mwandishi Wetu.
BENKI ya Biashara ya Tanzania (TCB) imejipanga kuendeleza mageuzi ya kidijitali ili kuongeza ujumuishi wa kifedha kwa wajasiriamali wadogo na wa kati, lakini katika upande wa ukuaji wa mizania ya kifedha, jumla ya mali za benki ziliongezeka kwa asilimia 25 hadi kufikia shilingi trilioni 1.74, na amana za wateja zilifikia shilingi trilioni 1.17, ikiwa ni ishara ya kuongezeka kwa imani ya wateja.
Haya yameelezwa leo Mei 26, 2025 jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TCB Martin Kilimba katika Mkutano Mkuu wa 33 wa wanahisa uliofanyika katika ofisi za TCB.
Amesema benki hiyo inaweka mkazo kwenye kuboresha miundombinu ya teknolojia ya kidijitali na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa makundi hayo muhimu ya uchumi, kwa lengo la kuchochea maendeleo ya sekta binafsi na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.
"Malengo yetu ni kuendelea kuboresha mizania, kujenga taswira mpya ya taasisi yetu, kutumia fursa zinazoletwa na teknolojia ya kidijitali, kufanya uhakiki wa hasara, pamoja na kusimamia rasilimali watu". Amesema
0 Comments