Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkuu wa Takukuru Protas Henry leo mei 8 Mwaka huu katika ofisi za takukuru ameeleza kuwa walibaini uwepo wa ubadilifu wa fedha kutoka kwenye vikundi 41 ambavyo havikukidhi vigezo ambavyo mikopo yake ilikuwa hewani.
Henry ameeleza kuwa vikundi hivyo vilibainiwa na makosa mbalimbali ikiwemo, kuomba mikopo Kwa Miradi hewa, kuwasilisha vielelezo vya kugushi kwenye kamati, kuwasilisha bei za juu za vifaa kuliko bei ya soko, kutokuwa na maeneo ya kufanyia biashara pamoja na kuomba mikopo Kwa ajili ya mradi wa mtu binafsi au familia.
Hata hivyo amefafanu kuwa TAKUKURU imechukua hatua ya udhibiti wa kuziba mianya yote ya rushwa iliyojitokeza ili kuisaidia Halmashauri hiyo ya Jiji la Mwanza kutoa mikopo Kwa vikundi vilivyokidhi vigezo.
"Vikundi 87 vilikidhi vigezo kati ya vikundi 128 viliomba mikopo ambapo jumla ya sh, Bi, 1,369,820,476 imeidhinishwa kutolewa Kwa ajili ya vikundi hivyo" Alisema Henry.
Aidha ameeleza kuwa kutokana na elimu wanayoitoa Kwa wananchi wameendelea kupata uelewa wa madhara ya rushwa na makosa ya rushwa .
"Uelewa huu umesaidia wananchi kufahamu wajibu walionayo katika kuzuia vitendo vya rushwa katika maeneo yanayowazunguka ikiwa ni pamoja na sehemu wanazopata huduma za kijamii hivyo kupelekea kuongezeka Kwa utoaji wa taarifa za vitendo vya rushwa" Alisema Henry.
Mwisho
0 Comments