NA MATUKIO DAIMA MEDIA
Wabunge wa Ulaya wamejadili maazimio kuhusu Mwenyekiti wa Chama cha upinzani, Chadema Tanzania, Tundu Lissu na kulaani kitendo cha kukamatwa kwake pamoja na tuhuma zinazomkabili ambazo ambazo wanasema zinaonekana kuwa za kisiasa na zinazobeba hatari ya kifo.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya bunge hilo kufanya kikao cha dharura kujadili suala la Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu.
Maazimio yaliyojadiliwa ni yapi?
Wameitaka Serikali ya Tanzania kumwachilia mara moja Lissu na bila masharti yoyote, ili kuhakikisha usalama wake na haki yake ya kusikilizwa kwa haki na uwakilishi wa kisheria.
Wabunge hao wanazitaka mamlaka za Tanzania kukomesha ukandamizaji unaoendelea, ukamataji hovyo, unyanyasaji, mashambulizi na unyanyasaji dhidi ya wanachama wa upinzani, watetezi wa haki za binadamu, watu wa kiasili, wanaharakati wa LGBTIQ+, waandishi wa habari na mashirika ya kiraia, na kuchunguza kwa uhuru dhuluma za polisi na kupotea kwa watu, kudumisha utawala, sheria, vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari na mahakama.
Sheria za uhalifu wa mtandaoni na vyombo vya habari za Tanzania kwa zizingatie sheria za kimataifa za haki za binadamu, kuheshimu haki za vyama vya siasa na kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki.
Wito kwa mamlaka za Tanzania kurejesha ushiriki kamili wa Chadema katika uchaguzi wa Oktoba 2025 na kushirikiana na vyama vyote vya siasa katika mazungumzo ya uwazi na jumuishi kuhusu mageuzi ya uchaguzi, kwa kushauriana na mashirika ya kiraia na wadau wengine.
Wito kwa EU na nchi wanachama wake kuwasiliana kwa kina na mamlaka za Tanzania kuhusu kesi ya Lissu na kufuatilia kwa karibu kesi; inawataka kuzingatia hatua zinazofaa ikiwa hali ya haki za binadamu itaendelea kuzorota.
Wanaitaka Tanzania kufuta hukumu ya kifo na kubadilisha hukumu zote za kifo.
Wanasisitiza haja ya EU kuhakikisha kwamba ushirikiano wake wa kimaendeleo na Tanzania, ikiwa ni pamoja na mpango wa Global Gateway, unaendana na uendelezaji wa haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na viwango vya kesi vyenye haki.
Wabunge hao wanamuagiza Rais wake kupeleka azimio hilo kwa Serikali na Bunge la Tanzania pamoja na Umoja wa Afrika.
Azimio hilo linatarajiwa kupigiwa kura na wabunge hao leo Alhamisi tarehe 8
chanzo:BBC
0 Comments