Header Ads Widget

WAZIRI RIDHIWANI KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE


 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA DODOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mheshimiwa Ridhiwani Jakaya Kikwete, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Kiwanda cha Saruji cha Dangote, waliomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma.


Ujumbe huo umeongozwa na Meneja wa Kiwanda hicho hapa nchini, Bw. Adeyemi Fajobi, ambapo mazungumzo yao yalijikita katika kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo na namna ya kuzitatua kwa pamoja.

Aidha, Waziri Ridhiwani aliwakumbusha wageni wake kuhusu umuhimu wa kiwanda hicho kwa Watanzania, hususan katika kutoa ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo Mkoa wa Mtwara ambako kiwanda hicho kipo.


Kwa upande wake, Bw. Adeyemi alimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa ushirikiano wa serikali, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kushughulikia changamoto zinazojitokeza mahali pa kazi. Pia aliomba serikali kuendeleza ushirikiano ili kuhakikisha mazingira bora ya uwekezaji na ajira.

Waziri Ridhiwani alimhakikishia kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kushirikiana na kiwanda hicho katika kuboresha mazingira ya kazi, kukuza ajira na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI