Header Ads Widget

IRINGA ROYAL CARS KUWANUSURU WATANZANIA KUTAPELIWA KWA KUAGIZA MAGARI NJE

 



NA MATUKIO DAIMA MEDIA 

CHANGAMOTO ya watanzania kutapeliwa pesa na madalali wa magari wasio waadilifu imepata ukombozi baaada ya kufunguliwa kwa ofisi ya uagizaji wa magari nje ya Iringa Royal Cars .

kufunguliwa kwa ofisi hii Iringa kutasaidia zaidi kila mwenye ndoto ya kumiliki gari kufanikiwa kwa uhakika zaidi badala ya kutuma pesa kwa mtu ama dalali usiyemtambua .

Watanzania waliowengi wamekuwa na uhitaji mkubwa wa kumiliki magari  uhitaji huu wa magari kutoka nje ya nchi umeongezeka kwa kasi kubwa, hasa kutoka Japan, Uingereza na Dubai 

Wakati miji mikubwa kama Dar es Salaam, Arusha na Mwanza ikiendelea kuongoza kwa uagizaji na uuzaji wa magari, Mkoa wa Iringa  na mikoa mingine nchini nao umeanza kuonesha dalili za kushamiri kwa sekta hii muhimu kupitia Iringa Royal Cars

Uchunguzi mdogo uliofanywa Matukio Daima Media  kwa kushirikiana na wadau wa usafirishaji na wauzaji wa magari unaonesha kuwa vijana na wawekezaji wa kati mkoani Iringa wameanza kuchangamkia fursa ya kuagiza magari moja kwa moja kutoka nje ya nchi.

 Lengo kuu ni kupunguza gharama kwa wanunuzi na kuleta ushindani kwenye soko ambalo hapo awali lilitegemea zaidi wauzaji kutoka mijini.

Katika muktadha huo, kampuni mpya inayojulikana kwa jina la Iringa Royal Cars imeanza kujizolea umaarufu na mvuto mkubwa kwa wakazi wa Iringa na mikoa ya jirani.

 Kampuni hiyo imejikita katika kuagiza magari moja kwa moja kutoka Japan, Uingereza na Dubai huku ikilenga kuwahudumia wateja kwa urahisi, kwa gharama nafuu na kwa kuaminika.


Akizungumza kupitia kipindi cha Tanzania ya Leo, Mkurugenzi wa Iringa Royal Cars, Benson Kimambo, amesema kampuni hiyo ilianzishwa kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kupata magari kutoka nje ya nchi kwa njia rahisi na salama.

“Shughuli hii imekuja baada ya kuona watu wengi wanatamani kuagiza magari kutoka nje, hasa Japan, lakini hofu imekuwa kubwa kutokana na utapeli unaoambatana na biashara hii Sisi tuliona kuna pengo hilo na tukaanzisha huduma ya uhakika kwa wakazi wa Iringa na maeneo ya karibu,” amesema Kimambo.

Mbali na hayo, Kimambo ameelezea changamoto kubwa wanayokumbana nayo  ikiwa ni upatikanaji wa dola za kimarekani, ambazo kwa sasa zinazidi kupanda thamani dhidi ya shilingi ya Kitanzania. 

Hata hivyo, Iringa Royal Cars imeanzisha mfumo rafiki wa malipo ya awamu, ambao unamwezesha mteja kulipia kidogo kidogo hadi atakapokamilisha kiasi kinachohitajika kwa ajili ya uagizaji wa gari lake.

Kwa upande wao, wakazi wa Mkoa wa Iringa wamepongeza  jitihada hizo, wakieleza kuwa kampuni hiyo inaleta matumaini mapya katika sekta ya usafiri na ujasiriamali katika mkoa huo.

“Mimi naona  kama fursa kubwa kwa wana Iringa. Kwa sababu sasa mtu anaweza kuagiza gari na kulipa kwa awamu. Ni jambo ambalo litawafungua watu wengi kiuchumi na kiakili,” amesema Martin Fernandz, mmoja wa wakazi wa Iringa.

Kwa kutambua umuhimu wa kushirikiana na serikali katika kukuza uchumi na maendeleo ya kijamii, Iringa Royal Cars pia imeahidi kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii, zikiwemo mbio za “Great Ruaha Marathon’’ ambazo hulenga kulinda mazingira ya mto Ruaha na kuhamasisha utalii wa ndani.

Iwapo unahitaji kuagiza gari leo wasiliana na Iringa Royal Cars piga  0713896681/0756542681

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI