Header Ads Widget

HUYU HAPA MGOMBEA URAIS NCCR-MAGEUZI


 Na Fatma Ally Matukio DaimaApp

Chama cha NCCR -  Mageuzi kimemsimamisha Mwenyekiti wa Chama hicho Haji Ambari Hamis kuwa mgombea Urais wa Tanzania Bara na Joseph Roman Selasini kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanya Octoba mwaka huu.

Aidha, kwa upande wa Zanzibar bado hawajachagua wagombea wa nafasi ya Urais, wapo katika mchakato

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo hii Katibu Mkuu wa Chama hicho, Evaline Wilbard Munisi amesema chama hicho kitashiriki kikamilifu katika uchaguzi huo huku akiwataka watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuchagua viongozi bora.

Amesema kuwa, miongoni mwa ajenda watakazo kwenda nazo katika uchaguzi huo ni pamoja na ajenda ya Uzawa, kwani wao wanaamini uchumi wa Taifa hilo ukiwa mikononi mwa wazawa basi vijana wataweza kupata Ajira lakini pia watalipa kodi kwa wakati.

Aidha, amesema zoezi la uchukuaji wa fomu za kugombea katika nafasi mbalimbali ikiwemo Ubunge na udiwani bado nafasi zipo za kutosha ni vyema watanzania wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu, ambapo zitaanza kutolewa tarehe 31 Mei hadi 15 June katika Ofisi za Chama hicho Ilala Jijini Dar es Salaam .

"Chama chetu kimejinga kushiriki kikamilifu kwa kusimamisha wagombea katika nafasi zote, udiwani, uwakikishi katika Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Ubunge katika bunge la JMT , Urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Urais wa JMT "amesema Evaline.

Sambamba na hayo wamewataka wapiga kura kutumia haki yao ya kikatiba kushiriki kikamilifu , hasa katika kupiga kura, ambapo takwimu zinaonyesha kwamba tangu mwaka 2000 katika uchaguzi mkuu ushiriki unakuwa ni mdogo, hii inachangiwa sana watu kukata tamaa.

Hata hivyo, ameiomba tume huru ya Taifa ya uchaguzi kuendelea kutoa ushirikiano katika kufanya zoezi la uchaguzi kuwa wa huru, amani na Haki kama ambavyo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameshatamka, huku wakiamiani elim ya Uraia ikitolewa kwa wapiga kura malalamiko yote yatasikilizwa kwa wakati.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI