Header Ads Widget

DKT SAMIA AMUENZI MAGUFULI KWA KUKAMILISHA MIRADI - MAKALLA

Na Matukio Daima App.

CHATO: Katibu Wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, CPA Amos Makalla amesema Rais Samia Samia Suluhu Hassan amemuenzi aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk John Pombe Magufuli kwa kukamilisha miradi yote ya kimkakati aliyoiacha ikiwa haijakamilika.

Makalla ameeleza hayo leo wakati akizungumza na wananchi katika eneo la Mganza katika Wilaya ya Chato mkoani Geita ikiwa ni muendslezo wa ziara yake ya siku saba katika mikoa sa kanda ya ziwa.

Makalla amesema Dk Magufuli aliongoza Tanzania vizuri na kuanzisha miradi mingi ya maendeleo na kufanya mambo mengi makubwa na kifo chake kilipelekea hofu na wasiwasi kwa watu juu ya utekelezaji wa miradi ya mikubwa ya kimkakati.

"Mungu akamjalia ujasiri Dk Samia Suluhu Hassan, hotuba yake ya kwanza bungeni aliahidi kwamba mimi nilikuwa msaidizi namba moja wa John Pombe Magufuli nawaahidi watanzania chochote alichoanzisha nitakikamilisha na mbali ya kukamikisha ipo miradi mingine nitaianzisha," amesema Makalla.

Akizungumza hayo Makalla ametaja miradi Rais Samia aliyoiendekeza likiwemo daraja la Kigongo - Busisi, kukamilishwa kwa hospitali ya Kanda, kutoa Sh bilioni 37 kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji katika miji 28 Chato ikiwa ni moja wapo, Sh bilioni 1.7 kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Samaki Chato Beach.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI