Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdul Kambaya (katikati) akimnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Makurumla, Ndugu Bakari Kimwanga (kulia) 12.10.2025 katika viwanja vya Mburahati Gine. |
Na. Mwandishi Wetu, Dar.
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdul Kambaya amemnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Makurumla, Ndugu Bakari Kimwanga ili awaletee maendeleo.
Awali akitoa neno katika mkutano huo, Kambaya amewataka Wananchi kuendelea kuwa na imani na Serikali iliyo chini ya CCM huku akiwataka wapinzani wenye hoja waje jukwaani.
"Wapinzani leteni hoja zenu tushindane kwenye uchaguzi.
Kama unazo hoja njoo mbele za Watanzania, na sisi CCM tutaleta hoja zetu mbele yao, Kisha watachagua, hoja zetu ama zenu, kwa kuwa hamshiriki uchaguzi basi tuacheni ili tuzungumze na Watanzania." Amesema Kambaya.
Na kuongeza:
"Mtu mwenye uwezo wa kutafakari hawezi kulishwa maneno kutoka katika mitandao ya kijamii, kwanza huna hakika lini utakutana naye, yupo hai ama amekufa, unauhakika kama anaipenda Tanzania ama haipendi?, Huyo mtu anakufanyia wewe kukuelekeza nini cha kufanya? hatuwezi kwenda hivyo". Amesema Kambaya.
Kambya amesema, CCM ina sera nzuri, imefanya mambo makubwa kila mtu anaimani na CCM ikiwemo kwenye Afya na shule na nyingine zimetekelezwa na Serikali ya CCM.
"Tujitokeze Oktoba 29 kumpa kura nyingi za Ndiyo Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge Mhe. Profesa Kitila Mkumbo na Diwani wetu hapa Bakari Kimwanga.
"Makurumla ya sasa imebadilika tofauti na zamani, kwani maendeleo ya barabara na miundombinu imeimarika.
Kwa upande wake, Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo ameomba kura nyingi za Ndiyo ili aendelee kuwa Mbunge wa Jimbo hilo, lakini pia ameomba kura nyingi za Ndiyo kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Diwani Bakari Kimwanga.
Prof Kitila Mkumbo ameweza kuelezea sifa kuu tatu za Rais ambazo mgombea wa CCM, Samia Suluhu Hassan anazo ni:
"Uongozi wowote duniani, unahitaji kiongozi imara.
Sifa ya Rais ni kuwa imara, mgombea wetu wa Urais ni imara.
Lakini pia Rais mwenye uelewa wa Uongozi wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa maana Tanzania Bara na Zanzibar.
"Naombeni kura zenu za Ndiyo Oktoba 29, tulete maendeleo katika elimu, Afya, Miundombinu na masuala ya Usalama.
"Kazi kubwa tunaenda kuifanya hapa kwenu Makurumla ni pamoja na kujenga kingo katika mto China.
Tunatambua shida inayowakabiri.
Pia kuna mito mingine ndani ya Jimbo letu hili ikiwemo mto Gide nalo inaenda kutatuliwa." Amemalizia Prof. Kitila Mkumbo
Nae, Mgombea Udiwani wa Kata hiyo, Ndugu Bakari Kimwanga amewahakikishia Wananchi hao waliojitokeza kwenye Mkutano huo uliofanyika Mburahati katika uwanja wa Gine, kuwa suala la kero ya maji inafanyiwa kazi na tayari watalaam wa Mamlaka husika wameweza kufika kwa hatua za ufumbuzi.
"Injinia wa maji DAWASA wamefika hapa kwa ufumbuzi, Mbunge na mimi mgombea Udiwani wenu tunatatua kero bila kuchoka.
Aidha, Bakari Kimwanga amesema kuwa, kuhusu kero ya mto China, ni kwamba wanaenda kujenga kingo zake kuzuia kero ya mafuriko msimu wa mvua.
"Shida za Wananchi zinatatuliwa na Chama Cha Mapinduzi CCM, tunawahakikishia utekelezaji na hatua tunaanza nayo ujenzi wa Kingo, lakini pia iwe mto umekufuata ama umeufuata Serikali imeonelea kutoa kifuta jasho ili kuachana vyema wakati wa ujenzi wake". Amesema Bakari Kimwanga.
Aidha, Bakari Kimwanga amejiombea kura na pia amemuombea kura Kitila na Rais Samia.
0 Comments