Header Ads Widget

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE: CUNHA TAYARI KUJIUNGA NA MAN UTD

Mshambuliaji wa Wolves Matheus Cunha anatarajiwa kujiunga na Manchester United baada ya msimu kukamilika wikendi hii huku klabu hiyo ya soka ya England iitarajiwa kuanzisha kipengele cha kutolewa kwa mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 kwa pauni milioni 62.5. (Sky Sports)

Manchester United pia imefanya mazungumzo ya ana kwa ana na mshambuliaji wa Ipswich Town na England Liam Delap, 22. (The Athletic)

Beki wa Bayer Leverkusen Jeremie Frimpong, 24, amekamilisha vipimo vyake vya afya katika klabu ya Liverpool siku ya Jumatatu. Tetesi zinasema mchezaji huyo wa Uholanzi alisafiri Uingereza siku ya Jumapili kufanikisha mchakato huo. (Sky Sports)

Aston Villa ina nia ya kumsajili mlinda lango wa Liverpool na Ireland Caoimhin Kelleher, 26, huku MArgentina Emiliano Martinez, 32, akitarajiwa kuondoka Villa msimu wa kiangazi. (Sun)

Manchester United, Barcelona na Saudi Pro League ni miongoni mwa klabu zinazofuatilia hali ya Martinez. (Sun)

Bayer Leverkusen imekadiria thamani ya kiungo wao wa kati wa Ujerumani Florian Wirtz, 22, kuwa pauni milioni 126 huku Bayern Munich na Liverpool wakimtaka baada ya Manchester City kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili. (The Times - usajili unahitajika)

Mkufunzi wa Sheffield Wednesday wa Ujerumani Danny Rohl, 36, anawania nafasi katika klabu ya Southampton. Muingereza Will Still, 32, pia yuko katika kinyang'anyiro hicho. (Sky Sports)

Marseille haina nia ya kumuuza mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Mason Greenwood, 23, lakini huenda ikalazimika kufany ahivyo kutokana na "hali ya kiuchumi". (RMC Sport)

Sunderland ina hamu ya kumsajili mlinzi wa Montpellier wa Mali Modibo Sagnan, 26 - endapo itashinda kupanda Ligi ya Premia kupitia mechi za mtoano au kusalia kwenye Ubingwa. (Sunderland Echo)

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI