Header Ads Widget

DC SWEDA:TEKNOLOJIA HAIEPUKIKI KWA SASA,JAMII ITUMIENI

 


          Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Serikali wilayani Njombe imewasisitiza wananchi kuendelea kutumia vyombo vya habari ili kupata taarifa sahihi na kukuza maendeleo yao kwani teknolojia kwa sasa haiepukiki kwa namna yoyote.


Mkuu wa wilaya ya Njombe Juma Sweda wakati akizindua duka la ving'amuzi vya kampuni ya Azam mjini Njombe amesema Teknolojia kwa sasa imeyafikia maeneo yote na kutoa ajira kupitia vyombo vya habari.


Kwa upande wao wananchi Mkoani Njombe wamesema vyombo vya habari vimekuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya taifa jambo ambalo jamii inapaswa kujua umuhimu wake na kuvitumia.


Jonas Mbaga ni Meneja mauzo wa Kanda ya nyanda za Juu kusini wa kampuni ya Azam ambaye mbali na kusogeza karibu huduma za kampuni hiyo lakini anakiri kuwa vyombo vya habari vinasaidia kuchagiza uchumi na kukuza biashara.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI