Na Shemsa Mussa -Matukio daima Kagera.
Mpamgo wa Mfuko wa Bima kwa wote kuwafikia Wananchi wa Mkoa kagera ,huku huduma nyingine zikiendelea kutolewa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF.
Akizungumza na Mwandishi Wetu akiwa ofisini kwake Meneja wa NHIF Mkoa kagera Ndg Ismail Nuhu Kangeta ,amesema kwa Sasa wapo katika hatua za mwanzo za ueilimishaji kuhusu huduma hiyo na hasa katika upande wa sheria muhimu zitakazozingatiwa katika utekelezaji wa huduma hiyo ya Bima kwa wote.
Amesema Bima kwa wote ni mpango wa Serikali ambao unatoa mwongozo kwa Kila mtu kuweza kupata huduma za Afya kwa ghalama nafuu, hasa kwa wakulima, Wajasiliamali,wavuvi,wafugaj, pamoja na Wafanyabiashara wadogo wadogo,pia kupitia huduma hiyo Serikali itatoa huduma za matibabu bure kwa wale wasio na uwezo kupitia huduma ya Bima jamii.
Amezitaja huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ni pamoja na ada ya kujiandikisha( kumuona Daktari) huduma za dawa,vipimo,upasuaji,Uzazi,kinywa na meno pamoja na ghalama za kulazwa,ikiwa ni moja ya dhima yao ya kusimamia taratibu za matibabu na kuhakikisha Kila mwanachama anapata huduma za matibabu pindi afikapo Hospitalini,ikiwa huduma hizo ni kuanzia kituo Cha Afya Hadi hospital ya Taifa.
Katika kuhakikisha NHIF inaendana na wakati, Meneja amesema kwa Sasa wanataka kuhama katika Mfumo wa Kila mwanachama kuja ofisini,na kuhamia katika Mfumo wa digital ambapo mwanachama ataandika na kujaza taarifa zake mwenyewe kupitia simu ya Mkononi (smart phone), hivyo kuwasisitiza wananchi wa Mkoa huo kuendelea kujiunga na Mfuko huo wa Bima ya Afya.
"Kama tunavyofahamu upatikanaji wa fedha ya pamoja ni mgumu sana na hasa wakulima na wananchi wengine vyanzo vyetu ni vigumu mno ila kama mkulima ukivuna mazao Yako ya msimu unatenga kiasi kidogo kwa ajili ya kulipia matibabu ndani ya mwaka mzima,sioni kama Kuna shida kubwa mtu kuwekeza katika Afya yake,mara nyingi tumekuwa tukikumbuka umuhimu wa Bima baada ya kupata magonjwa jambo ambalo sio,amesema Bw Kangeta "
Pia amekemea vitendo kwa baadhi ya wanachama kufanya udanganyifu wa kuweza kutumia kadi ya mtu mwingine ili kupata huduma za matibabu huku akisema katika kukabiliana na Hilo wanaendelea kuhamasisha na kusistiza matumizi ya (finger Print) kidole gumba ili kutokomeza changamoto hiyo,na ametoa tahadhari kwa baadhi ya watoa huduma za Afya kuwasilisha madai ambayo sio sahihi pindi mwanachama anapokuwa anapatiwa matibabu
0 Comments