Na WILLIUM PAUL, MOSHI.
KATA Mabogini katika Jimbo la Moshi vijijini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro ni miongoni mwa kata zilizofanikiwa kupokea fedha kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika Halmashauri ya Moshi.
Shule hiyo mpya ya Sekondari Mtakuja ilipokea fedha kiasi cha Shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya katika Kijiji cha Mtakuja.
Ujenzi wa wa shule hiyo ilijumuisha majengo ya madarasa, maabara, ofisi za walimu, jiko na bwalo.
Mradi huo umeboresha huduma za elimu ya Sekondari kwenye Kata ya Mabogini yenye sekondari mbili za kata, na wakazi zaidi ya elfu 557,231.
Shule hiyo imeondoa adha ya watoto kutembea umbali mrefu kufuata huduma za elimu kwenye shule za Sekondari za Mpirani na Mabogini zilizo mbali na makazi yao.
Anna Lyimo mkazi wa kijiji cha Mtakuja alisema alisema kuwa ujenzi wa shule hiyo umewezesha wanafunzi kutotembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu.
Alisama kujengwa kwa shule hiyo kutasaidia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Aidha aliishukuru Serikali kwa kutoa fedha za kutekeleza Mradi huu pamoja na Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini Profesa Patrick Ndakidemi na Diwani wa Kata ya Mabogini Bibianna Massawe kwa kuupigania mradi huu.
Mwisho..
0 Comments