Header Ads Widget

BAGAMOYO WAJA NA FILAMU YA BAGAMOYO PREMIER TOUR KUUTANGAZA UTALII MHESHIMIWA JAKAYA KIKWETE ATAHUSIKA

 

Baada ya Filamu ya Royal tour iliyoongozwa na kuratibiwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Sasa Bagamoyo waja na Bagamoyo Premier Tour Filamu ambayo Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete atahusika kutangaza vivutio vya utalii wa wilaya ya Bagamoyo ya mkoani Pwani ambayo itarushwa sehemu mbalimbali duniani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari na Wadau wa Utalii Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga katika ukumbi wa millennium sea breeze resort uliopo bagamoyo amesema ujio wa filamu fupi kuhusu utalii wa Bagamoyo utaonyesha uhalisia wa vivutio vya utalii wa aina mbalimbali kwa kushirikiana na Viongozi mbalimbali akiwemo Mheshimiwa Dkt. Kikwete, wabunge wa majimbo yote mawili ya Bagamoyo Mwalami Mkenge na Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete watahusika.

Filamu ya Bagamoyo Premier Tour ni filamu fupi yenye lengo la kuutangaza utalii wa bagamoyo kwa ukubwa kwani 

Hii ni Netflix certified documentary ambayo inaandaliwa na ofisi ya mkuu wa Wilaya bagamoyo pamoja na mtembezi adventures.

"Tunataka Dunia ijue bagamoyo tuna utajiri wa vivutio vya utalii"


Aidha mhe. Ndemanga amezungumzia swala la makampuni na wafanya biashara kujitokeza kushirikia katika maandalizi ya filamu hiyo kwani itakua fursa ya kujitangaza katika biashara zao.

Aidha amewaomba Watanzania na Wadau mbalimbali wa maendeleo kuwa sehemu ya maandalizi ya filamu kuhusu Utalii wa Bagamoyo inayotarajiwa kuanza hivi karibuni na akibainisha namna filamu hiyo itakavyoleta tija na mafanikio mkubwa katika suala la Utalii na Utamaduni wa  Bagamoyo.

Kwa upande wake mwandaaji wa filamu hiyo Samson Samuel amesema lengo la kuandaa filamu hiyo ni kutangazia Dunia juu ya Utalii uliopo wilayani Bagamoyo na kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika kutangaza Utalii ili kuongeza watalii hapa nchini.

Alisema Filamu hiyo itaelezea kwa kina vivutio vya utalii vilivyopo wilayani humo ikiwa ni pamoja na hifadhi peke ya Saadan inàyoungana na bahari ambapo  watalii na wanyama huweza kukutana kwenye beach ya bahari ya Hindi kuogelea, nyingine ni Hifadhi ya Wamimbiki, Magofu ya kale ya historia, kuangalia miamba mbalimbali ambayo ni vivutio na vivutio vingine mbalimbali.

Naye mwakirishi wa mmoja wa wadhamini Azania Banki Margreth Zungu amesema Banki hiyo itashiriki ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt Samia ambapo pia Banki hiyo itatangaza fursa na Huduma zinazotolewa na Azania Bank hapa nchini.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI