Header Ads Widget

ASKOFU DKT, CHILONGANI APEWA RUNGU KUKIONGOZA CHUO KIKUU CHA ST JOHN


 Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima App Dodoma 

ASKOFU  Mkuu wa Kanisa la Anglican Tanzania, Mahimbo Mndolwa ameongoza Ibada ya  kumsimika Mkuu wa chuo (Chancellor) wa pili wa Chuo Kikuu cha St John,Askofu Dk Dickson Chilongani.

Askofu Dk Chilongani ambaye ni Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika  anachukua nafasi ya Askofu Leonard Mtetemela ambaye amestaafu katika nafasi hiyo aliyoihudumu kwa kipindi cha miaka 18 tangu  Septemba 8,2007.

Ibada hiyo imefanyika leo Mei 20,2025   katika Chuo Kikuu cha St John Jijini hapa na kuhudhuriwa  na watu mbalimbali ambapo akizungumza katika ibada hiyo,Askofu Mndolwa amemtaka  Askofu Chilongani kwa kushirikiana na Kanisa kusimamia suala la mmonyoko wa maadili huku akihoji sera ya maadili ipo wapi.


“Ninyi wenzetu mpo sehemu za kuhoji ndio mtuongoze tunaomba idara ya Theolojia msogee mbele zaidi mmefundisha theolojia sasa tuende kwenye utafunaji wa hoja,hakuna njia ya kulirudisha kanisa isipokuwa kwa njia hiyo ya kupaza sauti,”amesema Askofu Mndolwa 

Kwa upande wake Mkuu mpya wa Chuo hicho,Dk Chilongani amesema  atapambana kwa kushirikiana na wenzake kuhakikisha chuo hicho kinazidi kupanda kitaaluma Pamoja na suala la mmonyoko wa maadili kwa kuhakikisha wanaozalishwa wanakuwa mfano katika jamii.

“Nimepokea chuo kikiwa katika hali nzuri ya kitaaluma nitahakikisha nashughulikia kwa kina changamoto ya ukosefu wa hosteli ili wanafunzi wakae sehemu nzuri na kuweza kujisomea vizuri,”amesema  Askofu Dk Chilongani.

mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI