Header Ads Widget

ALIYEKUWA WAZIRI MKUU WA TUNISIA AFUNGWA JELA KWA TUHUMA ZA UGAIDI

 

Ali Laarayedh alikuwa waziri mkuu muongo mmoja uliopita

Mahakama nchini Tunisia imemhukumu Waziri Mkuu wa zamani Ali Laarayedh kifungo cha miaka 34 jela kwa msururu wa mashtaka ya ugaidi.

Yeye ndiye mkosoaji mkuu wa hivi punde zaidi wa rais kufungwa jela huku wanakampeni wakikosoa "mashitaka ya uongo" nchini humo.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 69 ni mpinzani mashuhuri wa Rais Kais Saied na kiongozi wa chama maarufu cha Ennadha - kikubwa zaidi bungeni - ambacho kinakuza itikadi za Kiislamu.

Pamoja na watu wengine saba, Laarayedh alishtakiwa kwa kuanzisha kundi la kigaidi na kuwasaidia vijana wa Tunisia kusafiri nje ya nchi kujiunga na wapiganaji wa Kiislamu nchini Iraq na Syria.

"Mimi si mhalifu... mimi ni muathirika katika kesi hii," aliandika katika barua kwa mwendesha mashtaka wa mahakama mwezi uliopita, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Alihukumiwa siku ya Ijumaa.

Laarayedh amekuwa akikana kosa lolote na kusema kuwa kesi hiyo ilichochewa kisiasa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI