Hamida Ramadhani Matukio Daima APP Dodoma
WAZIRI wa kilimo, Hussen Bashe, amelaani madai kwamba chai ya Tanzania haiuziki duniani, na kueleza wazi kuwa huo ni uzushi mkubwa.
Akizungumza leo Aprili 8,2025 kwenye mkutano mkuu wa wadau wa tasnia ya chai, Bashe amefichua kwamba uchunguzi wake umeonyesha kuna mahitaji makubwa ya chai ya Tanzania, lakini viwanda vyetu vinakabiliwa na changamoto za ubora.
Waziri Bashe amesisitiza kuwa, umuhimu wa kuboresha mchakato wa uzalishaji ili bidhaa yetu iweze kushindana kimataifa.
"Tunahitaji kushirikiana kwa thati kabisa kama wadau ili kuimarisha tasnia hii ya chai hapa nchini,"
Alisema Bashe, akiongeza kuwa soko la chai linakua kwa kasi na kuna fursa kubwa za kiuchumi.
Amehimiza matumizi ya teknolojia ya kisasa na mafunzo kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji na viwango vya ubora.
"Tukifanya kazi pamoja, tunaweza kufikia malengo yetu na kuleta maendeleo katika sekta hii ya zao la chai," amesema
Naye Mwenyekiti wa bodi ya Chai Tanzania Abdulmajid Nsekela amesema anahitaji kuoana sekta ya chai inakuwa na kuchangia pato la nchi na hata kwa mtu moja mmoja
"Hii iko wazi moja ya kazi sekta binafsi ni pamoja na kuleta mabadiliko chanya na ndio maana leo hii tupo hapa lengo kuu ni kuhakikisha tunafanya au kuendesha chai kibiashara zaidi, " Amesrma
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya Rungwa Jafari Haniu amesema Wilaya hiyo imekuwa ikulima chai lakini wakulima wa Rungwe wamekuwa na kulio cha kila siku bei ndogo ya majani mabichi ya chai.
Kilio kingine cha wakulim wa Rungwe ni pamoja kucheleweshwa kwa mlipo hadi muda wa miezi sita.
"Hivyo kupitia mkutano huu naomba utoke na majibu juu ya wakulima hawa kwani wengine wanadiriki kutaka kuniletea familia zao nizitunze kwani wao tegemeo lao ni kilimo cha zao la chai huku kilio kingine kikiwa ni mashamba kutelekezwa,"Amesema Mkuu wa wilaya huyo
0 Comments