Header Ads Widget

KESHO SIMBA INAHITAJI NGUVU YOTE,HAKIKISHA UKO UWANJANI_ SIMBA INAKUSUBIRI!!

 


“Kesho hatakiwi kubaki Mwanasimba yoyote kubaki nyumbani. Kama watu wametoka Mbeya, wengine Tunduma, wengine Mwanza, wewe wa Temeke unafanya nini nyumbani, unaacha kuja kuungana na Wanasimba yoyote uwanjani.”

“Kila zama zina kitu cha kujivunia, sisi zama za sasa ni kuipeleka Simba nusu fainali. Imetosha sasa kujivunia historia ya 1993, imetosha kujivunia historia ya 2003. Kwa timu tuliyonayo hili linawezekana na HII TUNAVUKA.”

“Ni wakati sasa wa kuandika historia yetu ili tujivunie. Na wenzetu wa zamani kuna kazi kubwa waliifanya ili kufanikiwa, na moja ya kazi walifanya ni kuujaza uwanja wa Shamba la Bibi, watu waliingia saa 2 asubuhi pale. Na tunaenda kutoa machozi na damu kwa kununua tiketi na kuujaza uwanja, na sisi kesho tunakwenda kuandika historia yetu.”- Semaji Ahmed Ally akiongea katika uzinduzi wa Tawi la Simba la Azimio, Tandika.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI