Header Ads Widget

WATU NI WALEWALE "MAVUNDE VS BASHE"


Na. Andrew Chale, Matukio Daima App Dar.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na msemo wa 'Watu ni walewale' ambao binafsi nimehusikia kwa Naibu Waziri Mkuu, Mhe Dotto Biteko akielezea namna harakati zake za kisiasa akiwa UVCCM, na wakati huo pia alitolea mfano DC wa Kahawa Mhe Mboni akiwa akiwa Makamu wa Jumuiya na sasa yeye ni Naibu Waziri Mkuu na Mboni ni Mkuu wa Wilaya.

Matukio Daima App imeshuhudia andiko la Mbunge Dodoma, Mhe Anthony Mavunde alitolea mfano kama huo ila kwa UPANDE wake katika harakati za kugombea nafasi za UVCCM Taifa, kwa wakati huo, zaidi yeye na Hussein Bashe.

Alichoandika Mhe Mavunde:

"Mwaka 2008 niligombea Uenyekiti wa UVCCM mkoa Dodoma,na nafasi ya Makamu Mwenyekiti Vijana CCM Taifa ilikuwa inagombewa na Ndg. Beno Malisa na Hussein Bashe,mimi sikumuunga mkono Bashe nilikuwa kwa Beno.

Kwakuwa Dodoma ilikuwa sehemu muhimu ya kimkakati ya kufanikisha ushindi.Bashe akamuunga mkono mpinzani wangu kwakuwa alijua nikishinda hatapata kura za mkoa wa Dodoma.Bahati nilishinda na nikamtumia ujumbe kwamba namsubiri kwenye uchaguzi wake.

Ilipofika wakati wake siku moja kabla ya Uchaguzi wa UVCCM Taifa, wagombea wakiwa kwenye Treni kutoka Mwanza waliandaa mapokezi yao stesheni ya Dodoma kwa kuwa treni ilikuwa inabeba zaidi ya asilimia 50 ya wapiga kura wote.


Nilihakikisha  Bashe hapati mapokezi makubwa Dodoma na badala yake iwe ni Beno hivyo nikakodi vikundi vyote vya tarumbeta na mdundiko.

Bashe alipofika Manyoni anawapigia watu wake akaambiwa hakuna hata kikundi kimoja kipo kumsupport,akili ya haraka ikamjia akakodi Music System kutoka NK Disco Tech,muziki ule ukawa mkubwa kuliko sauti ya vikundi vyangu hivyo nikaamuru watu wangu waucheze muziki uliokodiwa na Bashe kwa kuimba jina la Beno😂😂😂.

Ikatokea vurugu kubwa kati ya watu wa Beno na Bashe,tukaamuriwa na Polisi kwa msaada wa Mkuu wa Mkoa wakati huo akiwa Mh. William Lukuvi.

Tukaenda kwenye uchaguzi Beno akashinda ila tukabaki na mpasuko wa Team Beno na Team  Bashe,hivyo ikapelekewa kuundwa Timu maalum ya kuipitia upya UVCCM kurejesha amani na umoja ambayo ilipelekea mapendekezo ya kutungwa kanuni mpya ya UVCCM inayotumika sasa.Katika Timu hiyo Bashe alikuwa Mwenyekiti na mimi nilikuwa Makamu wake, 𝐓𝐔𝐊𝐀𝐎𝐌𝐁𝐀𝐍𝐀 𝐑𝐀𝐃𝐇𝐈 𝐓𝐔𝐊𝐀𝐒𝐀𝐇𝐀𝐌𝐄𝐀𝐍𝐀.

Mwaka 2012 wakati nagombea Umakamu Mwenyekiti UVCCM Taifa na UNEC- UVCCM ,Bashe alikuwa mstari wa mbele kuniunga mkono na amebaki kuwa 𝐤𝐚𝐤𝐚 na 𝐫𝐚𝐟𝐢𝐤𝐢 wa kweli wa muda wote.

Mwaka 2022 Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan akamteua Hussein Bashe kuwa Waziri wa Kilimo na mimi kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Najiluliza tusingekuwa 𝐓𝐔𝐌𝐄𝐒𝐀𝐌𝐄𝐇𝐀𝐍𝐀 pale Wizarani pangekuwaje?

𝐓𝐮𝐯𝐮𝐦𝐢𝐥𝐢𝐚𝐧𝐞,𝐓𝐮𝐩𝐞𝐧𝐝𝐚𝐧𝐞 𝐧𝐚 𝐓𝐮𝐬𝐚𝐦𝐞𝐡𝐚𝐧𝐞  𝐤𝐰𝐚𝐬𝐚𝐛𝐚𝐛𝐮 𝐤𝐞𝐬𝐡𝐨 𝐧𝐢 𝐟𝐮𝐦𝐛𝐨 𝐤𝐮𝐛𝐰𝐚.

𝐖𝐀𝐓𝐔 𝐍𝐈 𝐖𝐀𝐋𝐄 𝐖𝐀𝐋𝐄

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI