Header Ads Widget

BREAKING :MSAFARA WA MWILI WA KATIBU WA UWT MBEYA,WAPATA AJALI DODOMA

 


Na Habari na Matukio App,Dodoma 

Msafara unaosindikiza mwili wa marehemu Lucia Sulle aliyekuwa Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Mkoa wa Mbeya umepata ajali Kijiji cha Haneti Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wakati wakielekea Mkoa wa Manyara kwa ajili ya shughulu ya mazishi.

Kwa mujibu wa taarifa za mashuhuda, ajali hiyo imehusisha lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 832 EBU lenye tela lenye namba za usajili T 732 EJW na Costa lililokuwa limebeba mwili wa marehemu lenye namba za usajili T 267 EBM.

Mganga Mfawidhi Dr. Ramadhani Msigala ambaye amewapokea majeruhi katika kituo cha afya ameeleza hali ya majeruhi .


Matukio Daima Tv tumemtafuta kamanda wa polisi wa mkoa wa Dodoma amesema yupo ziara ila atafuatilia na kutoa taarifa kamili ya ajali hii .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI