Header Ads Widget

WATAALAM MRADI WA SOFF WAPOKEA, WAPITISHA BAJETI 2025

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Ladislaus Chang’a Kamati Tendaji ya Mradi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuimarisha Uangazi wa Hali ya Hewa (SOFF) imepokea na kupitsha mpango kazi na bajeti kwa mwaka 2025.

Dk. Chang'a ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), alisema hayo wakati akifungua rasmi mkutano wa pili wa kamati tendaji ya SOFF mjini Morogoro jana Aprili 10, 2025.

“Moja ya masuala yatakayojadiliwa katika kikao cha pili cha Kamati Tendaji ya Utekelezaji wa Mradi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuimarisha Uangazi wa Hali ya Hewa (SOFF) ni pamoja na kutathimini utekelezaji wa mpango kazi wa mwaka 2024, kupokea na kupitsha mpango kazi na bajeti kwa mwaka 2025”.


Aliendelea kuishukuru kamati hiyo pamoja na sekretarieti kwa kazi kubwa iliyofanyika katika kuhakikisha majukumu ya mradi kwa mwaka 2024 yanatekelezwa kwa ufanisi ikiwemo hafla ya uzinduzi wa mradi huo.

Dk. Chang’a alifafanua TMA iliandaa mpango kazi wa utekelezaji wa maelekezo matano yaliyotolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi yakiwemo masuala ya utekelezaji wa shughuli za mradi kwa wakati na ufanisi na ushirikiano wa wadau wa mradi.

Awali wakati wa ufunguzi, Naibu Mwakilishi Mkazi Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Amos Manyama alisisitiza kuwa UNDP itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania, TMA na Wadau wengine wa mradi kuhakikisha malengo ya SOFF yanafikiwa. Aidha aliendelea kusisitiza haja ya kuendelea kuimarisha ushirikiano na TMA katika kuimarisha huduma za haki ya hewa hata baada ya mradi.


Katika hatua nyingine, Kamati ilipokea na kuidhinisha Mpango Kazi wa mwaka 2025, taarifa ya hesabu kwa mwaka 2024 na mpango wa Ufuatiliaji na tathmini wa mradi.

SOFF ni Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuimarisha Uangazi wa Hali ya Hewa kwa Nchi zinazoendelea na Nchi za Visiwa vidogo. Lengo la Mradi ni kuimarisha huduma za hali ya hewa katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi ili kulinda maisha ya watu na mali ikiwemo kuboresha zaidi miundombinu ya uangazi wa hali ya hewa na kuhakikisha Tanzania inakidhi mahitaji ya wadau.

Mwishoooo.....

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI