Header Ads Widget

TETESI KUBWA 5 ZA SOKA ULAYA JIONI HII: BAADA YA MO SALAH SASA VIRGIL VAN DIJK

 


Mohamed Salah amemaliza uvumi kuhusu hatma yake kwa kusaini mkataba mpya na Liverpool. (Skysport)

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 sasa ameweka kalamu kwenye mkataba ambao utamweka Anfield hadi 2027.

Ni jambo kubwa kwa Liverpool huku Salah akiwa na kiwango kizuri msimu huu, na kuisaidia klabu hiyo kukaribia kutwaa taji lao la 20 la ligi.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri ameisaidia Liverpool kuwa kileleni mwa Ligi Kuu ya England akiwa amefunga mabao 27 na kutoa asisti 17.

Salah ameshinda Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa, Kombe la FA na Vikombe viwili vya Ligi pamoja na Kombe la UEFA Super Cup, Kombe la Dunia la Klabu ya FIFA huko Liverpool.

Salah anasema "Bila shaka nimefurahi sana," aliambia tovuti rasmi ya Liverpool. "Tuna timu kubwa sasa. Kabla pia tulikuwa na timu kubwa. Lakini nimesaini kwa sababu nadhani tuna nafasi ya kushinda mataji mengine na kufurahia soka langu.

Mlinzi wa timu hiyo, Virgil van Dijk nae atasaini mkataba mpya wakati wowote baada ya kufikia makubaliano na Liverpool.

Shangilia ya Ekitike dalilia ya kutua Arsenal?

Henry na Ekitike (kulia)

Mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike amekoleza tetesi za uhamisho wake kuelekea Arsenal! baada ya kuchapisha picha inayofananisha ushangiliaji wake unaofanana kabisa na ushangiliaji wa nguli wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry dhidi ya Tottenham (Goal.com)

Alichapisha picha hiyo baada ya mchezo dhidi ya Tottenham Hotspur. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22, alianza kuifungia Eintracht Frankfurt katika pambano lao la Ligi ya Europa dhidi ya Hotspur Alhamisi usiku kwa bao kali, lakini ni shangwe yake ambayo ilivutia macho ya mashabiki wa Arsenal, wakisema ni dalili anatajiunga Arsenal.

"Tuna namba tisa" - Enzo Maresca


Kocha wa Chelsea, Enzo Maresca anasema: "Namba tisa yangu iko kamili kabisa na ni Nico Jackson. Tayari tuna namba tisa".

"Na kwa kuwa sasa Sasa si kipindi cha majira ya kiangazi. Kama tunaweza kupata anayefanana na Nico, basi sawa. Nimesema mara nyingi, na mnaweza kuona pia, tukiwa na Nico timu yetu huwa bora zaidi. Nico ndiye tunayemhitaji". (Chelsea Press)

Roma yamtaka Vieira kama Kocha mpya

Nahodha wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira anafikiriwa kuwa kocha mpya wa Roma, kulingana na Sky nchini Italia.

Vieira kwa sasa ni kocha wa Genoa na amewaongoza hadi nafasi ya 12 kwenye ligi.

Sky nchini Italia wanaripoti kwamba Stefano Pioli, Maurizio Sarri na Vincenzo Montella pia wanazingatiwa, huku Vieira akiwa wa nne kwenye orodha hiyo.

Vieira alistaafu soka mwaka wa 2016 na amekuwa meneja katika klabu ya New York City FC inayoshiriki Ligi ya MLS, Nice kwenye Ligue 1, Crystal Palace, Strasbourg na Genoa tangu 2024.

Barcelona yamtaka mlinda mlango wa Real Sociedad Remiro

Kwa mujibu wa Catalunya Radio, Barcelona inamuania mlinda mlango wa Real Sociedad Alex Remiro ambaye amepangwa kuwasili Camp Nou siku zijazo.

Ripoti hiyo inasema kwamba mawasiliano tayari yamefanywa na wawakilishi wa kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 kuhusu uhamisho hapo baadaye.

Huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania akiwa na kandarasi hadi 2027, inaelezwa kwamba uhamisho wa 2026 unawezekana kwa Barcelona kutokana na bei ya Remiro kupunguzwa.

Remiro amekuwa na Real Sociedad tangu 2019, na amekuwa akiimarika kila msimu.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI