Header Ads Widget

WACHAKATAJI MAZAO YA UVUVI KIGOMA WALIA MAENEO YAO KUZAMA




Na Fadhili Abdallah,Kigoma

WAJASILIAMALI wanawake  wachakataji wa mazao ya uvuvi katika  Mwalo wa Muyobozi Mwambao wa Kusini wa ziwa Tanganyika halmashauri ya wilaya Uvinza mkoani Kigoma wameeleza kuathirika kiuchumi baada ya maeneo yao ya kufanyia kazi kumezwa na maji .

Wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mradi wa kutoa mafunzo ya kuongeza thamani kwa mazao ya uvuvi na elimu ya biashara mradi unaoendesha na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Muyobozi Environment Concervation Wanawake hao wamesema kuwa kwa sasa hawana maeneo maalum ya kufanyia shughuli zao.




mmoja wa wajasiliamali hao, Pili Salum alisema kuwa mazingira ya kazi ni magumu kwani mabadiliko ya tabia nchi yaliyosababisha kuongeza kwa maji katika ziwa Tanganyika imefanya maeneo yao ya uchakataji kujikuta yamezingira na maji ikiwemo maeneo ya kuanikia dagaa na samaki.

Naye mchakataji mwingine, Elizabeth Pius alisema kuwa awali wakati maeneo yao yameboreshwa walikuwa wanafanya kazi kwa pamoja wadau wote wa uvuvi wakiwemo wavuvi, wauzaji wa mazao ya uvuvi na wachakataji lakini kwa sasa hali ni ngumu kila mmoja ametafuta eneo la kujistiri ili shughuli zake ziweze kwenda.

Kufuatia hali hiyo wameiomba serikali kuwatafutia eneo lingine ambalo litaboreshwa na kuwekewa miundo mbinu itakayowezesha shughuli zao kufanyika kwa tija ikiwemo maeneo ya kuanikia mazao yao ya uvuvi.

Akizungumzia kadhia hiyo, Mratibu wa mpango wa kuwajengea uwezo wanawake kuhusu uchakataji wa mazao ya uvuvi ili kuyaongezea thamani kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Muyobozi Environment Conservation,Kessi Yakuti alisema kuwa pamoja na mradi huo pia wanaangalia namna ya kushirikiana na serikali kukabiliana na hali hiyo inayowakumba wadau wa uvuvi.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI