Header Ads Widget

VISIWA VYA FALKLAND NAVYO VYAHISI MAUMIVU YA USHURU WA MAREKANI



Ushuru mkubwa uliotangazwa na rais wa Marekani Donald Trump sio tu unaathiri uchumi wa nchi zenye Uchumi mkubwa kama Uingereza na Canada – Uchumi mdogo pia zinahisi hivyo, ikiwa ni pamoja na Visiwa vya Falkland.

Idadi ya watu isiyo zidi 3,700 wanaishi kwenye visiwa vya mbali vya Atlantiki Kusini.

Sasa wanatazamia athari ya ushuru wa 42%.

Janet Robertson, meneja mkuu wa kampuni ya Consolidated Fishing Limited, anaiambia BBC World Service kwamba Marekani ni soko kuu la bidhaa zake.

"Tunashangaa yote yataishia wapi," Janet anasema.

Uvuvi "kwa sasa ni sekta muhimu zaidi katika visiwa vya Falklands", anaongeza.

"Uuzaji wa bidhaa zitokanazo na Samaki katika taifa la Marekani umekuwa na mchango mkubwa, ambapo kwa kiasi fulani ndiyo sababu tumeishia kuwekewa ushuru huu mkubwa kulingana na viwango vya ushuru visivyo vya kawaida ambavyo vimebuniwa na Marekani.’’

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI