Header Ads Widget

MAANDAMANO YA KUMPINGA TRUMP YANATARAJIWA MAREKANI NA LONDON

 



Wakati waziri mkuu wa Uingereza akijipanga kuhusu namna ya kukabiliana na ushuru wa Trump, umati wa watu unakusanyika kote Marekani kuandamana.

Maandamano yamepangwa kufanyika katika majimbo yote 50 na Washington DC leo, huku watu wakiazimia kumpinga Rais Donald Trump na sera zake.

Kumekuwa na maandamano ya mara kwa mara tangu aingie madarakani, lakini waandaaji wanasema wanatarajia leo kuwa siku moja kubwa zaidi ya maandamano tangu Trump aanze muhula wake wa pili.

Makumi kwa maelfu ya Wamarekani wanatarajiwa kushiriki katika matukio nchini kote - na kuna maandamano yaliyopangwa London na miji mingine ya Canada na Ulaya pia.

Wakati huo huo waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer anaripotiwa kutumia wikendi hii kuzungumza na viongozi wa kigeni kuhusu hatua ya ushuru.

Tayari alizungumza na wenzake wa Australia na Italia jana usiku.

Downing Street inasema viongozi wote watatu walikubaliana kwamba "vita vya biashara vya pande zote vitasababisha hasara kubwa sana".

Kwa mujibu wa ofisi hiyo maafisa wa Uingereza "wataendelea kwa utulivu na kazi ya maandalizi, badala ya kukimbilia kulipiza kisasi".

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI