Maafisa wa uokozi katika Jamhuri ya Dominican sasa wanaelekeza nguvu katika kutafuta miili na sio tena kuokoa walioangukiwa na paa la ukumbi wa burudani siku mbili zilizopita wakati wa tamasha la muziki.
Miili mia moja na ishirini na nne imetolewa kutoka klabu ya Jet Set.
kwa siku mbili familia zimekusanyika nje ya mabaki ya klabu ya Jet Set huko Santo Domingo, zikihangaikia taarifa kuhusu jamaa zao waliopotea na kushiriki picha na polisi ili kusaidia katika utambuzi.
Maafisa hao wa uokozi wanasaidiw ana timu ya Israel na Mexico ambao wanatumia vifaa vya hali ya juu vya kutafuta joto kujaribu kupata mtu yeyote ambaye bado yuko hai.
Madai yameanza kuibuka kiini cha anguko la paa hilo ambalo limeua watu 184.
Wengi wananyooshea kidole cha lawama tukio la moto lililotokea katika klabu hiyo ya burudani miaka miwili iliyopita.
Wengine wanahofia kuwa moto huo ulidhoofisha nguzo za jengo hilo na kuhofia kuwa huenda ukarabati uiofanywa baada ya mkasa haukuafiki viwango hitajika.
Mmiliki wa klabu hiyo ya Jet Set, Antonio Espaillat, alitoa ujumbe wa video kupitia mitandao ya kijamii akieleza rambirambi zake na zile za "familia yote ya Jet Set", kwa jamaa za wahasiriwa.
Pia alisisitiza kuwa yeye na timu yake walikuwa wakishirikiana "kabisa na kwa uwazi na mamlaka" juu ya janga hilo.
Msanii maarufu Rubby Perez aliyekuwa akitumbuiza ni miongoni mwa waliofariki.
Serikali imetangaza siku tatu za maombolezo.
0 Comments