Header Ads Widget

MBUNGE GHATI CHOMETE AWAOMBEA MAJI WANANCHI WA KATA ZA BISUMWA,NYANKANGA NA BUKABWA WILAYA YA BUTIAMA


Na Shomari Binda-Musoma 

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mara Ghati Chomete amewaombea upatikanaji wa maji wananchi wa Kata za Bisumwa,Nyankanga na Bukabwa zilizopo Wilaya ya Butiama.

Maombi ya mbunge huyo ameyatoa leo April 8 bungeni katika kikao cha kwanza cha mkutano wa 19 wa bunge la bajeti alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwenye Wizara ya Maji.

Kabla ya kuuliza swali hilo mbunge huyo ameishukuru serikali kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maji ili kuwezesha wananchi kupata maji kwenye maeneo yao.

Amesema miradi hiyo imewezesha kumtua mama ndoo kichwani na kumshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwaajili ya miradi hiyo.

" Mheshimiwa Naibu Spika nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kwenye Wizara ya Maji.

" Kwanza naidhukuru serikali kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji kwa mkoa wa Mara,swali langu ni lini wananchi wa Kata za Bisumwa,Nyankanga na Bukabwa wilayani Butiama watafikishiwa huduma ya maji?",ameuliza

Akijibu swali la mbunge huyo Naibu Waziri wa Maji Kundo Mathew amempongeza mbunge huyk kwa ufatilisaji wake kwa kuwasemea wananchi.

Amesema serikali inaendelea kuwafikia wananchi kwa huduma ya upatikanaji wa maji na maeneo ambayo yametajwa na mbunge huyo yatafikiwa.

Naibu Waziri huyo amesema mradi mkubwa wa Mugango-Kiabakari hadi Bitiama umekamilika na umeanza kutoa huduma na utazifikia Kata hizo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI