Header Ads Widget

TDB KUANZISHA BAR ZA MAZIWA NCHINI ILI KUKUZA UNYWAJI WA MAZIWA.

Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima App Dodoma

BODI ya Maziwa Tanzania (TDB) imebuni mkakati mpya wa ubunifu kwa lengo la kuhamasisha unywaji wa maziwa nchini kwa  kuanzisha bar za maziwa.

Akiongea katika kikao kazi cha watumishi wa bodi hiyo kikao kilicholenga kukuza na kuendeleza Tasnia ya maziwa  Profesa George Msalya Msajili wa bodi ya maziwa amesema Mpango huu unalenga kuwavutia Watanzania wa rika zote, hasa vijana, ili kuongeza kiwango cha unywaji wa maziwa kama sehemu ya maisha yao ya kila siku.

Prof. Msalya amesema bar hizo za maziwa zitakuwa maeneo maalumu ambapo wananchi wataweza kufurahia aina mbalimbali za maziwa na bidhaa zake kama vile mtindi, siagi, maziwa ya ladha tofauti, pamoja na vinywaji baridi vyenye virutubisho vya maziwa.

"Uanzishaji wa baa hizi ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kuongeza matumizi ya maziwa kwa kila mtu, ambayo bado ni ya chini ukilinganisha na viwango vinavyopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO),"Amesema.

Na kuongeza "Hata hivyo, matarajio ni kueneza bar hizo Mijini hadi maeneo ya vijijini kadri uelewa na mahitaji ya maziwa unavyozidi kuongezeka," Amesema .

Mbali na kuongeza unywaji wa maziwa, bar hizi pia zinatarajiwa kutoa ajira kwa vijana, kuongeza soko kwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa, na kuimarisha uchumi wa sekta ndogo ya maziwa nchini. 

"Hii inakwenda sambamba na ajenda ya taifa ya uchumi wa viwanda na kilimo chenye tija," Amesema.

TDB inawahimiza wananchi wote kuunga mkono mpango huu, na kuona maziwa si tu kama kinywaji cha asubuhi, bali kama sehemu ya maisha ya kila siku. 

Kwa upande wake Kaimu Katibu mkuu Dkt, Charles Mhina akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Rizuki Shemdoe amewataka watumishi ho kutoka kwenye Tasnia ya maziwa kuzingatia misingi mitatu ya maadili ikiwemo Weledi, ikiwanipamoja na kuzingatia utaalamu na ubora wa maziwa ili walaji wasipate madhara. 

Pia amewataka watumishi hao waaminifu kuepuka wizi, kutunza vifaa vya ofisi . 

Sambamva na hilo amewataka watumishi hao kutunza siri za ofisi na kuacha tabia za kusema mambo ya serikali kwaamana yupo msemaji wa serikali. 


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI