Header Ads Widget

SERIKALI YAONGEZA MISHAHARA KIMA CHA CHINI KWA ASILIMIA 23.3

 

NA HAMIDA RAMADHAN,MATUKIO DAIMA APP DODOMA

SERIKALI imeongeza mshahara wa kima cha chini kwa asilimia 23.3, ikizingatia uwezo wa kibajeti na hali ya uchumi wa nchi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Aprili 17,  2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma.

Aidha, Serikali imetoa nyongeza ya mwaka ya mshahara (Annual Increment) kwa watumishi wa umma kwa mwaka wa fedha 2023/24 na 2024/25 ambapo Nyongeza hiyo inalipwa kila mwezi kulingana na tarehe ya mwisho ambayo mtumishi alipandishwa cheo

Pia amesema Serikali imelipa malimbikizo ya mshahara ambapo hadi kufikia tarehe 31 Machi, 2025 madai ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi 130,463 yenye jumla ya Sh. 226,584,818,810.18 yalipokelewa na kushughulikiwa. 

Aidha amesema ,katika kipindi hicho, madai ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wastaafu 10,022 kutoka kwa waajiri yenye jumla ya Sh. 33,290,109,780.75 yamepokelewa na kushughulikiwa na wahusika wamelipwa kupitia kwa waajiri wao.

"Mpaka kufikia tarehe 31 Machi, 2025, jumla ya watumishi wa umma  610,733 wamepandishwa vyeo, 42,515 wamebadilishwa kada, 3,208 wamepata uteuzi, 157,512 wamesafishiwa taarifa zao za kiutumishi, 10,725 wamebadilishiwa vyeo, 3,877 wamerekebishiwa majina, 9,269 wamefanyiwa mabadiliko ya mshahara binafsi, 2,558 wamerejeshwa kwenye utumishi wa umma na 133,317 wameajiriwa katika Taasisi mbalimbali za umma,"Amesema Waziri Simbachawene. 

Ameeleza kuwa, katika kipindi hicho, Jumla ya nafasi za ajira 149,000 zimetolewa na jumla vibali vya ajira mbadala 39,934 vimetolewa ili kujaza nafasi zilizobaki wazi kwa sababu mbalimbali.

AmesemaKuundwa kwa Mfumo wa Huduma Mtandao kwa Watumishi (Watumishi Portal) umewawezesha Watumishi wa Umma kupata huduma mbalimbali za kiutumishi moja kwa moja bila kulazimika kwenda kwenye Ofisi za Waajiri wao. 

"Mfumo huu pia unawezesha watumishi wa Umma kuomba mkopo kutoka kwenye Taasisi za kifedha kwa njia ya Mtandao," Amesema.

 Na kuongeza "Pia watumishi wanaweza kutafuta watumishi wa kubadilishana vituo vya kazi kwenye mfumo, kuomba uhamisho kutoka kituo kimoja kwenda kingine au Taasisi moja kwenda nyingine, kuomba likizo, kuangalia hati ya mshahara (salary slip) na kuangalia wasifu wa mtumishi (my profile)," Amesema.


Katika kipindi cha kuanzia Mwaka 2020 hadi Mwezi Agosti, 2024, Ofisi imefanya uhamasishaji wa Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma kwa taasisi za Umma 88 kwa jumla ya Watumishi 3,443 kutoka katika Mikoa ya Mbeya, Mtwara, Mwanza Arusha na Kilimanjaro. 

Amesema Mazoezi hayo ni mwendelezo wa jitihada zilizochangia kukua kwa kiwango cha uadilifu kwa watumishi wa umma kama ilivyobainishwa kupitia utafiti uliofanywa na Ofisi mwaka 2022 kuhusu hali ya uadilifu katika utumishi wa umma, ambapo utafiti ulibainisha kuwepo kwa ongezeko la 9.8% kutoka 66.1% (2014) hadi 75.9% (2022);

Hata hivyo Kupitia Mfumo wa e-Mrejesho, Ofisi imepokea mrejesho jumla ya hoja 146,204, ambapo hoja 144,222 zilishughulikiwa na hoja 1,313 zinaendelea kushughulikiwa kupitia Idara na Vitengo. 

Utaratibu huu umeleta mafanikio makubwa ambapo uwajibikaji umeongezeka kwasababu ya urahisi wa ufuatiliaji kupitia mifumo ya TEHAMA, na wananchi wameongeza imani yao kwa Serikali kutokana na namna wanavyohudumiwa na kupata mrejesho kwa njia rafiki zinazowapunguzia gharama za usafiri kwa ajili ya ufuatiliaji;.

Ofisi imeendelea kushirikiana na Taasisi Simamizi za Maadili kwa kuzijengea uwezo Kamati za Uadilifu kupitia Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji kwa awamu ya III na sasa ya IV, ambapo katika kipindi cha Kuanzia Mwaka 2020 hadi Mwezi Agosti, 2024 Ofisi imezijengea uwezo Kamati za Uadilifu 59 zenye jumla ya watumishi (Wajumbe) 700 kwa njia ya  mafunzo ya Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma ikiwa ni sehemu ya kuimarisha nidhamu, utendaji kazi na uwajibikaji.

 "Ushirikiano huo umechangia mafanikio ya nchi kudhibiti vitendo vya rushwa.

Katika kipindi cha kuanzia Mwaka 2020 hadi Mwezi Agosti, 2024 Taasisi 275 katika Utumishi wa Umma zilijengewa uwezo kuhusu uzingatiaji wa  Sheria,  Kanuni  na  Taratibu kwenye  ushughulikiaji  wa  masuala  ya Kiutumishi," Amesema. 

Aidha, Taasisi 543 zilikaguliwa kwa lengo la kuangalia uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia masuala ya Kiutumishi; 

Ajira mpya

Katika kupambana na upungufu wa ajira, Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ilifanikisha mchakato wa Ajira na kuwapangia vituo vya kazi jumla ya waombaji kazi 55,162  Aidha, waombaji kazi waliopangiwa vituo vya kazi waliongezeka kutoka 7,659 mwaka 2020 hadi 20,158 mwaka 2024, sawa na ongezeko la asilimia 163.19 . 

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI